Maneno ya mke wa Marehemu wiki tatu baada ya msiba wa Deo Filikunjombe



Tanzania bado iko kwenye majonzi  baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo Haule Filikunjombe pamoja na Rubani Captain William Silaa na watu wengine wawili Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule waliofariki kwenye ajali ya Helikopta kwenye mbuga ya Selous.
Marehemu Deo Haule Filikunjombe ameacha mke na watoto, ambapo siku chache zilizopita kupitia kwenye akaunti ya instagram mke wa marehemu Filikunjombe, Saraha ameyaandika kuhusu vitu ambavyo vilikuwa vikizungumzwa hasa kwenye mitandao mbalimbali.
Za siku wapendwa nawashukuru wote kwa text nyingi za pole mlizonipa na kuwa pamoja na familia yangu kwa kipindi hiki kigumu kwetu kwa kumpoteza mtu muhimu katika maisha yangu nilizoea kumuita majina mazuri yote ila yale yote ntayahamishia kwa wanangu ulioniachia nawahakikishia nitasimama sehemu zote mbili kama baba na kama mama nitakupenda daima mume wangu Deo wangu Filikunjombe wangu jembe langu‘ -Saraha
novemba 09
Nawashukuru pia wale waliomsema vibaya mume wangu hakika malipo ni hapa hapa duniani ni mbaya sana kurukia jambo usilolijua nimekutana na marehemu mwaka 1999‘ – Saraha
Akiwa mwanafunzi wa chuo cha Makerere Uganda na kufunga nae ndoa 2003 akiwa polisi tulitamani maisha mazuri ila tulishindwa kutokana na ugumu wa maisha tumefanya mambo mengi mpaka kuwa hapa leo ikiwakupiga picha na baadaye tukafungua duka la camera kwa kuanza na kamera tatu tu na juhudi ndio iliyomfikisha alipo ishia anayeikashifu nyumba ungejua tulivyoijenga kwa shida usingesema nasema haya kwa maumivu makali sana leo’ – Saraha
kaiacha hajakaa hata wiki mbili angekuwa na hela siangeijenga zamani leo tungekuwa tumeichakaza ndo akafa naombeni ukiona mtu kapata shida jua namna ya kumfariji sio kuendelea kumuumiza asanteni wote by mjane wa Filikunjombe’ – Saraha
Za siku wapendwa nawashukuru wote kwa text nyingi za pole mlizonipa na kuwa pamoja na familia yangu kwa kipindi hiki kigumu kwetu kwa kumpoteza mtu muhimu katika maisha yangu nilizoea kumuita majina mazuri yote ila yale yote ntayahamishia kwa wanangu ulioniachia nawahakikishia nitasimama sehemu zote mbili kama baba na kama mama nitakupenda daima mume wangu deo wangu filikunjombe wangu jembe langu nawashukuru pia wale waliomsema vibaya mume wangu hakika malipo ni hapahapa duniani ni mbaya sana kurukia jambo usilolijua nimekutana na marehemu mwaka 1999 akiwa mwanafunzi wa chuo cha makerere uganda na kufunga nae ndoa 2003 akiwa polisi tulitamani maisha mazuri ila tulishindwa kutokana na ugumu wa maisha tumefanya mambo mengi mpaka kuwa hapa leo ikiwakupiga picha na baadaye tukafungua duka la camera kwa kuanza na kamera tatu tu na juhudi ndio iliomfikasha alipo ishia anaeikashifu nyumba ungejua tulivyoijenga kwa shida usingesema nasema haya kwa maumivu makali sana leo kaiacha hajakaa hata wiki mbili angekuwa na hela siangeijenga zamani leo tungekuwa tumeichakaza ndo akafa naombeni ukiona mtu kapata shida jua namna ya kumfariji sio kuendelea kumumiza asanteni wote by mjane wa filikunjombe
A


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: