Ikiwa ni siku chache toka shirikisho la soka barani Ulaya UEFA litangaze majina 40 ya wachezaji waliofanikiwa kuingia katika Top 40 ya wachezaji wanaowania kuunda kikosi cha wachezaji bora Ulaya, lakini list hiyo haikuwa na majina ya wachezaji kutoka katika klabu ya Manchester United hata mmoja.
November 26 shirikisho la kimataifa la wachezaji Professional FIFPro linalotambulika naFIFA limetangaza majina 55 ya mwisho yatakayowania kuunda kikosi bora cha Duniakwa mwaka 2015, majina yatakayofanikiwa kuunda kikosi hicho yatatangazwa 11 January 2015 wakati wa utolewaji wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or jijini Zurich Uswiss.
Katika list ya majina hayo 55 Uingereza imefanikiwa kuingiza wachezaji wawili pekeeWayne Rooney na John Terry wakati mfalme wa assist Mesut Ozil hakufanikiwa kuchaguliwa kuingia katika list hiyo. Mchakato huo ulianza ukiwa na majina 25,000 kutoka katika nchi 70 kabla ya November 26 kutangaza majina 55 pekee.
Hii ndio list ya majina yote 55 mtu wangu
Magolikipa (5): Gianluigi Buffon (Italia/Juventus), Iker Casillas (Hispania/Porto),David De Gea (Hispania/Manchester United), Keylor Navas (Costa Rica/Real Madrid)na Manuel Neuer (Ujerumani/Bayern Munich).
Mabeki (20): David Alaba (Austria/Bayern Munich), Jordi Alba (Hispania/Barcelona),Jerome Boateng (Ujerumani/Bayern Munich), Daniel Carvajal (Hispania/Real Madrid), Giorgio Chiellini (Italia/Juventus), Dani Alves (Brazil/Barcelona), David Luiz(Brazil/Paris Saint-Germain), Diego Godin (Uruguay/Atletico Madrid), Mats Hummels(Ujerumani/Borussia Dortmund), Branislav Ivanovic (Serbia/Chelsea), Vincent Kompany (Ubelgiji/Manchester City), Philipp Lahm (Ujerumani/Bayern Munich),Marcelo (Brazil/Real Madrid), Javier Mascherano (Argentina/Barcelona), Pepe(Ureno/Real Madrid), Gerard Pique (Hispania/Barcelona), Sergio Ramos(Hispania/Real Madrid), John Terry (Uingereza/Chelsea), Thiago Silva (Brazil/Paris Saint-Germain) na Raphael Varane (Ufaransa/Real Madrid).
Viungo (15): Thiago Alcantara (Hispania/Bayern Munich), Xabi Alonso(Hispania/Bayern Munich), Sergio Busquets (Hispania/Barcelona), Eden Hazard(Ubelgiji/Chelsea), Andres Iniesta (Hispania/Barcelona), Toni Kroos (Ujerumani/Real Madrid), Luka Modric (Croatia/Real Madrid), Andrea Pirlo (Italia/New York City), Paul Pogba (Ufaransa/Juventus), Ivan Rakitic (Croatia/Barcelona), James Rodriguez(Colombia/Real Madrid), David Silva (Hispania/Manchester City),Yaya Toure (Ivory Coast/Manchester City), Marco Verratti (Italia/Paris Saint-Germain) na Arturo Vidal(Chile/Bayern Munich).
Washambuliaji (15): Sergio Aguero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale(Wales/Real Madrid), Karim Benzema (Ufaransa/Real Madrid), Douglas Costa(Brazil/Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid), Zlatan Ibrahimovic(Sweden/Paris Saint-Germain), Robert Lewandowski (Poland/Bayern Munich),Lionel Messi (Argentina/Barcelona), Thomas Muller (Ujerumani/Bayern Munich),Neymar (Brazil/Barcelona), Arjen Robben (Uholanzi/Bayern Munich), Wayne Rooney(Uingereza/Manchester United), Alexis Sánchez (Chile/Arsenal), Luis Suarez(Uruguay/Barcelona) na Carlos Tevez (Argentina/Boca Juniors).
BOFYA HAPA CHINI KUJUA MIKOA AMBAYO MAGUFULI ATAFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KUANZIA SASA
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment