Kocha wa Tottenham Hotspur, Muargentina Mauricio Pochettino amewaambia Chelsea kujiandaa kisaikolojia endapo watatuma bid ya kutaka kumsajili mshambuliaji wake Harry Kane January hii kwa kuwa hawatakubaliwa.
Harry Kane ambaye yuko katika kiwango bora hivi sasa jana aliisaidia timu yake ya Tottenham alipoifungia goli dhidi ya Qarabag katika michuano ya Uropa ligi huku akitarajiwa kuivaa Chelsea Jumapili hii katika muendelezo wa ligi kuu nchini England, katika uwanja wa White Hart Lane.
Taarifa zinasema klabu ya Chelsea inajiandaa kutuma ndoano ya kumnasa star huyo katika majira ya dirisha dogo la usajili mwezi Januari ili kukiimarisha kikosi chao, lakini mocha Mauricio Pochettino anasema Chelsea watapoteza muda kufanya hivyo kwani Kane anataka kuisaidia Spurs kufuzu michuano ya klabu bingwa barani Ulaya sanjari na kushinda makombe akiwa White Hart Lane.
Harry Kane aliongeza mkataba unaomuweka klabuni halo hadi 2020 huku kukisemekana mazungumzo yanaendelea ku-improve mkataba wake ili kumfanya awe comfortable kuichezea time hiyo.
Kocha Pochettino amesisitiza kuwa anaamini Kane atafuata nyayo za golikipa Hugo Lloris aliyekataa ofa ya kujiunga na Manchester United mwezi Julai na kubaki White Hart Lane, huku akitaka Kane aipotezee Chelsea.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment