CAF YATOA 10 BORA MCHEZAJI BORA WA MWAKA



SAMATTA-KIKWETEJANA CAF imetoa 10 Bora ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Afrika kwa Makundi yake Mawili na Straika mahiri wa Tanzania, Mbwana Samatta, yumo.

Samatta, ambae huchezea Klabu ya Congo DR TP Mazembe ambayo ameifikisha Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI, yumo kwenye 10 Bora ya Wachezaji wanaogombea Tuzo hii kwa Wachezaji wanaocheza ndani Afrika.

Samatta ndie anaongoza Listi ya Wafungaji Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI akiwa na Bao 7 baada ya Majuzi kufunga Bao la ushindi wakati TP Mazembe inaichapa 2-1 USM Alger huko Algeria kwenye Mechi ya Kwanza ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Timu hizo zitarudiana huko Lubumbashi Jumapili inayokuja.
Washindi wa Tuzo hii huamuliwa kwa Kura za Makocha wa Timu za Taifa za Nchi Wanachama wa CAF.

Washindi hao watatangazwa Alhamisi, Januari 7, 2016 huko Abuja, Nigeria.

MCHEZAJI BORA WA MWAKA – WANAOCHEZA NDANI YA AFRIKA:
Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)
Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)
Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)
Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)
Mbwana Aly Samatta (Tanzania & TP Mazembe)
Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)
Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)
Roger Assalé (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)
Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)


MCHEZAJI BORA WA MWAKA:
André Ayew (Ghana & Swansea)
Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)
Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
Mohamed Salah (Egypt & Roma)
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
Sadio Mané (Senegal & Southampton)
Serge Aurier (Cote d’Ivoire & Paris Saint Germain)
Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)
Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)
Yaya Touré (Cote d’Ivoire & Manchester City)


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: