BETRAM MWOMBEKI TENA UWANJANI


MWOMBE
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Betram Mwombeki atajiunga na timu ya ligi daraja la tatu Mkoani kwao Mwanza wakati huu ambao ameamua kumpumzika kucheza ligi kuu. Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Alhamis hii akiwa Mwanza, Mwombeki amesema uamuzi wake huo umetokana ‘ kuuchukia’ mpira wa Tanzania pia kujishughulisha na shughuli zake za ufugaji na kilimo.
“Mungu akijalia nitarudi tena uwanjani, lakini sitajiunga na timu ya ligi kuu wala ligi daraja la kwanza licha ya kwamba kuna timu kadhaa zinanihitaji. Nitajiunga na timu ya ligi daraja la Tatu hapa Mwanza” anasema mchezaji huyo ambaye hakudumu zaidi ya msimu mmoja katika klabu ya Simba licha ya kuonyesha uwezo mkubwa katika utengenezaji wa magoli na ufungaji akicheza sambamba na Mrundi, Amis Tambwe msimu wa 2013/14.
“Kuna mambo yamenifanya nichukie sana mpira wa upinzani kwa hiyo nataka cheza mpira wa furaha bila mambo mengi pia nitaweza fanya mambo yangu mengine bila tatizo” Mwombeki alitanga kuachana na mpira wa ushindani mwaka uliopita baada ya kuona mpira wa Tanzania una matatizo mengi ya kiutawala



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: