Kocha wa klabu ya Arsenal mfaransa Arsene Wenger amelalamikia sheria za shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya, UEFA kuhusu dawa za kuongeza nguvu kwa wachezaji ‘doping’ kuwa zinasapoti matumizi ya dawa na wala haziondoi.
Arsene Wenger ameyasema hayo kutokana na shirikisho hilo kumfungia kucheza soka mchezaji Ademi (24) wa Dinamo Zagreb kwa miaka 4 kutokana kufeli vipimo vya dawa za kuongeza nguvu ‘drugs’ katika mchezo dhidi ya Arsenal mwezi September mwaka huu katika mechi ambayo Arsenal ilipoteza kwa goli 2-1.
Katika kuelekea mchezo wa marudiano leo usiku, Arsene Wenger amesema ameshtushwa na kitendo cha UEFA kupitia kitengo cha kupinga madawa kumfungia Ademi na kutowanyang’anya matokeo waliyoyapata ili kutoa fundisho kwa wengine.
Arsene Wenger anasema Dinamo Zagreb walitakiwa kupokwa ushindi na kufutwa kujihusisha na soka ili kuleta funzo kwa timu zingine lakini akalalamikia uamuzi wa kumfungia mchezaji pekee kuwa hakutasaidia kuondoa tatizo hilo.
Arsenal inaingia katika mchezo ambao wanahitaji matokeo kwa udi na uvumba ili kujipa matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku wakiiombea mbaya Olympiakos Pireus ipoteze mchezo wake dhidi ya Bayern Munich.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment