MSIMU uliopita, Manchester United waliongoza 3-1 huko King Power Stadium na kujikuta wakitandikwa 5-3 na Leicester City katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Septemba 21, 2014 na Jumamosi Timu hizi zinakutana Uwanja huo huo.
Safari hii, Leicester City, ndio Vinara wa Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 1 mbele ya Man United iliyo Nafasi ya Pili.
Mwaka Jana, Straika wa Leicester, Jamie Vardy, alifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi na kutengeneza zote 4 walipoifunga Man United 5-3, na safari hi indie anaongoza kuwa Mfungaji Bora wa Ligi.
Safari hii, Leicester wapo chini ya Kocha Claudio Ranieri ambae mara ya mwisho alifukuzwa akiwa Kocha wa Greece baada ya Nchi hiyo kufungwa na Vibonde wa Ulaya Faroe Islands.
++++++++++++++++++++++++++++
Ranieri, akisifika kama ‘Tinkerman’, yaani mbadilisha Kikosi kila kukicha,na mlolongo wa Klabu/Nchi alizowahi kufundisha [Na pia kutimuliwa]:
1986–1987 Lametini
1987–1988 Puteolana
1988–1991 Cagliari
1991–1993 Napoli
1993–1997 Fiorentina
1997–1999 Valencia
1999–2000 Atlético Madrid
2000–2004 Chelsea
2004–2005 Valencia
2007 Parma
2007–2009 Juventus
2009–2011 Roma
2011–2012 Inter Milan
2012–2014 Monaco
2014 Greece
2015– Leicester City
++++++++++++++++++++++++++++
Je Man United watakubali kupigwa 5 na Leicester kubaki kileleni?
Hilo ndilo swali la Wachambuzi wengi huko England lakini wengi, safari hii, hawaipi nafasi Leicester.
Wengi, wanadai, udhaifu wa Man United kwenye Difensi, ukichangiwa na Penati tata 2 na Goli tata 1, ndio uliwapa Leicester ushindi huo.
Wengi wa Wachambuzi hao wanadai mwisho wa Leicester kuselelea kileleni unaanza sasa kwani kati ya Jumamosi na Mwaka mpya Mechi zao ni dhidi ya Vigogo ambao ni Man United, Swansea, Chelsea, Everton, Liverpool na Man City.
KWA LISTI HII, LEICESTER ATANUSURIKA KWELI?
LIGI KUU ENGLAND:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 28
1800 Aston Villa v Watford
1800 Bournemouth v Everton
1800 Crystal Palace v Newcastle
1800 Man City v Southampton
1800 Sunderland v Stoke
2030 Leicester v Man United
Jumapili Novemba 29
1500 Tottenham v Chelsea
1705 West Ham v West Brom
1915 Liverpool v Swansea
1915 Norwich v Arsenal
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment