Lowassa,Viongozi Wa Ukawa Wamuaga Dk.Emmanuel Makaidi

Mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa akimuaga Mwenyekiti wa NLD Dk.Emmanuel Makaidi katika uwanja wa Karimjee jijini Dares salaam leo.
Mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa,Mgombea Mwenza Juma Duni Haji leo wameungana na wananchi, ndugu na jamaa kumuga mwenyekiti mwenza wa Ukawa Dk.Emmanuel Makaidi aliyefaliki dunia akiwa mkoani Mtwara.
Aidha, Dk. Makaidi, ambaye pia Mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD) alichokianzisha mwaka 1992, na mgombea ubunge jimbo la Masasi mkoani Mtwara, alifariki dunia Alhamisi wiki iliyopita katika hospitali ya Nyangao, Masasi, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).
Mara baada ya kuuuaga mwili huo katika uwanja wa Karimjee shughuli ya mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 74 itahitimishwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye katika eneo la kumuaga mwenykiiti mwenza Ukawa Dk.Emmanuel Makaidi.

Viongozi wa Ukawa wakiwasili kwenye uwanja wa Karimu jee kumuaga mwenyekiti Mwenza Ukawa Dk.Emmanuel Makaidi.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko


0 comments:
Post a Comment