SECONDARY SCHOOL
Sehemu Ya 17
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
Baada ya masaa kadhaa kupita sherehe ilikua imekwisha. sasa mama alikua kawasindikiza marafiki zake kwa kutumia gari...
Sasa nilipomuona zai nikamfuata na kumshika mkono huku nikimburuza mpaka geto kwangu huku nikiwa na hasira hio duuu...
Nilimfikisha hadi geto kisha nikambwaga kitandani kwangu kisha nikaanza kuvua mkanda wangu
"heee sheby? unataka kunifanya nini sheby?"
"tuliaaa, nyie si mnaniona mi hanisi si ndio?"
"sheby una nini wewe? hebu kumbuka mi ni dada yako sheby"
SONGA NAYOO
Nilikua sitaki kuskia kauli yake ya kua ni dada yangu. Niliuvua mkanda kisha nikauweka sawa kwa ajili ya kuchapa mtu,
"yaani usiponambia, huu mkanda utakuishia mwilini wote"
"sasa nikuambie nini?"
"hio sherehe inamuusu nani?"
"mmhhhh mi sijuiii"
"aaahaaa hutaki kusema si ndio?"
"subiri kwanza sasa"
"sema sasa"
Nilikua nimekua mkali ghafla ili tu nijue hio sherehe ni ya nani na inahusu nini... coz kila ninaemuuliza pia hawataki kunijibu kwa usahihi ulionyooka. but zai najua yeye ndio kipenzi cha mama hivyo najua tu atakua kaambiwa kuusiana na hii sherehe ya ghafla ghafla hivi...
"mama aliniambia kua, wewe kuna kitu umefanya ofisini..kwaio ndio maana kakuandalia sherehe kwa hicho ulichokifanya ofisini na secretary wetu"
Aliposema tu hivyo yaani kila kiyngo kilinilegea huku nikijiuliza kimoyo moyo kua
"kwanini mama anapenda mi niwe mzinifu?"
Nilijiuliza lakini sikujipatia jibu hata kidogo
"sepa zako basi"
Nilimfukuza zai chumbani kwangu huku nikichukua taulo na kwenda bafuni.. .Nilioga chapu chapu maana nilikua nachelewa msikitini kusali. maana wamenichelewesha na haya masherehe yao..... Nilimaliza kuoga kisha nikatupia kanzu na kibaraka shee. Kisha nikawa natoka zangu huku nikihesabu tasbii yangu.. Nilipotoka nje ya geti nilikutana na wasichana kama 6 hivi.. wakali kinoma
Kama kawaida yangu nikawasalimia kiislamu warembo hao
"Assalam Aleykh?"
"poa tu mambo zako?"
"kama amuezi si mtulie tu kuliko kuharimu salamu?"
Nilianza kuwagombeza kwakua hawakuitikia salamu yangu ya kiislamu
"we mkaka mbona una gubu wewe? kwani ni lazima tuitikie hio salamu yako?"
Mara zai akatokea huku kajitanda vizuri
"Eee ushaanza misele saa hizi mtoto wa kike watoka kwenu"
"heeee sasa nisiwasindikize marafiki zangu"
"sasa utarudi na nani usiku huo?"
"si wewe apo"
"mschiuuuuuuu mwehuuu nini wewe? yaani niache kwenda msikitini eti niwasindikize nyie? ivi hilo neno umeongwaa au umeropokwa?"
"ah ah mimi nawasindikiza hawa halafu mi nakuja kukusubiri pale nje ili ukitoka turudi wote"
"kama utaweza kusubiri hadi saa 5"
"heeee sheby saa 5 unafanya nini huko?"
"aaaa ebu nenda ukooo"
Waliondoka zao huku mimi nikitembea kwa miguu taratiiibu kabisa, kwani siku hio sikutaka kua na baiskeli, Hivyo nilikua sloo moo.. Nilipofika msikitini nilitawadha vizuri kisha nikaingia masjidi na kuswali swala ya saa 12 ambayo ilinipita
Baada ya kumaliza kulipia swala hio Nilichukua mswahafu na kuanza kujisomea maana nilikua nimeshaumaliza hivyo nilikua naurudia tu. Nilikua naisubiria swala ya INSHA yaani swala ya saa 2 usiku... Ilifika mida hio kisha nikaswali na baada ya hapo tukasoma dua mbili tatu za kweda kulalia...
Baada ya dua waislamu wote tukawa tunaagana kwa kutakiana kheri ya siku ijayo..
Basi nilitoka zangu pale masjidi na kuangaza angaza pembeni kama ningemuona zai. maana si alisema atanisubiria...
Sasa kutazama maeneo flani kwenye mti niliona wasichana wawili na mmoja wao alikua ni zai ila mwingine sikua namfahamu.
"we zai?"
Nilimuita kwa umbali huku kama nikianza safari ya kurudi nyumbani.
"abeee?"
"twende sasa"
akawa anakuja na yule rafiki yake. ila huyo rafiki yake sikua namjua kwani alikua kajitanda na mitandio kibao...
"mambo sheby?"
"alinisalimia huku akiwa bado kajifunika kanga usoni...
"safi tu, kwani we nani?"
Nilimuliza huku nikimuona zai kama anamsukuma sukuma aongee.....
Sasa uzuri ni kwamba na mimi pia ni jeuri na ni mtu mwenye zarau kwa yule mwenye zarau na mimi. Niliivuta ile kanga yake na kumuona sura. Alikua ni aisha.. kama unakumbuka kuna siku nilikutana nae nikiwa naelekea masjidi usiku...
"kwanini umejifunga na wakati sio taipu yako?"
Nilimuuliza huku nikijichekesha mwenyewe coz nashangaa sana kwa hawa watoto wa kike wanaonifata kwa njia tofaut tofaut
"nilitaka kujaribu kua unampenda nani kati ya msichana wa kiislamu na yule ambae ni wa kawaida"
"hahahaha mimi wote siwapendi"
"kwanini sasa sheby?"
Sasa maongezi yakiendelea baina yangu na aisha nilishangaa kumuona dada zai katangulia mbele Eti aniachie nimtongoze aisha. Niliona tu zai anajipa tabu tu. maana hizo swaga za kutongoza mimi hua sinaga kabisa..... kwanza hata kutongoza yenyewe sijui
"mwenye tu hua siwapendi"
"au walikutenda nini sheby?"
Sasa mtoto alikua keshaanza kunisogelea karibu huku akinigusa gusa ili nijiskie mwerere...
Afu sauti yake kaishua kabisa yaani anaongea na pua kama kudeka si kudeka. yani kakaakaa kimahaba mahaba tu.
"wala tu...sema mi siwapendi kabisa"
"sasa sheby??"
"nini?"
Mtoto wa kiume nilikua nakaribia nyumbani, ila aisha yeye kapitiliza kwao kwa ajili ya mimi
"mi nakupenda sheby?"
"Enhe ivi wewe? unaakili kweli?"
"lakini hujaniuliza huo upondo upoje"
"najua huo upendo wako"
"lakini sheby??? kwani we hujawai kuwa na mpenzi?"
"na sitaki kuwahi"
"basi naomba niwe wa kwanza kwako"
Aliongea utumbo wake huku nikitembea kwa spidi kuelekea getini kwetu... maana tulikua tumeshafika nyumbani sasa ile nataka kuingia. Nilishangaa nimezuiwa kwa mbele na aisha huku akiwa kanishika tai... sijakaa vizuri mara kanisogezea mdomo.
"sheby? unajua naumia sana juu yako, so plz naomba unipoze japo na denda tuuu plz nakuomba"
Sijakaa vizuri mara dada zai katokea huku akisema
"mpe mtoto wa watu kaka heee mpaka afe?"
baada ya kuongea hivyo afu akaingia zake ndani,
Sasa ile namuangalia zai kugeuka huku kwa aisga... Aisee nilikutana na mdomo lainiiii ulionifanya nishindwe kujitoa katika kinywa hicho
Sasa maskini mtoto wa kiume hata denda tu sijawahi kula... sasa mtoto alikua ananilazimishia
Sasa ile nakubali tu kula denda Nilishtukia nimepigwa kibao cha mkono. huku nikisikia sauti ikisema kua
"nani kakufunza huu upuuzi?"
Nilishangaa kusikia hio sauti na wakati kila siku naambiwa mimi sio riziki
Je? Ni nani huyo alieongea maneno hayo?
0 comments:
Post a Comment