KUMBE NI KOSA KUMTONGOZA MWANAMKE KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK, KIJANA WA MIAKA 20 AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA KOSA LA KUTONGOZA.


Mwanaume mmoja 20, aliyetumia Facebook kumtongoza mwanafunzi mwenza kwa nia ya kushiriki ngono naye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini Marekani.

Owen Labrie alipatikana na hatia ya kumtongoza msichana huyo ambaye jina lake limebanwa kwa sababu ya umri wake mdogo wa miaka 15.

Labrie na msichana huyo walikuwa wanafunzi wa shule moja ya kifahari sana mjini Concord, New Hampshire.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo, wakili wa mshtakiwa alidai kuwa ni desturi ya wanafunzi wanaokamilisha masomo kuwaalika wanafunzi wapya shuleni humo kisha wakashiriki ngono nao katika tamaduni inayojulikana kwa jina la uzushi ''kupiga saluti''

Shule hiyo ya kifahari na ghali ya St Paul inajivunia kuwa kitovu cha elmu kwa mamia ya viongozi wa kada mbalimbali nchini Marekani akiwemo waziri wa maswala ya kigeni John Kerry.

Wanafunzi wengine waliosomea katika shule hiyo ya ''Kupiga saluti'' ni mabalozi 13 na watafiti wenye hadhi ya juu duniani. 


Wakili wa msischana huyo aliiambia mahakama kuwa Labrie alijigamba kwa maswahiba wake kuwa alikuwa 'amepigia saluti' msichana huyo na hivyo kumsababishia fedheha miongoni mwa wanafunzi wake.

Katika kujitetea wakili wa Labrie aliomba mahakama imhurumie mteja wake kwani huo ulikuwa ujinga wa matineja waliokuwa mbioni wakitaka kukubalika na wenzao.

Jaji wa mahakama ya juu Larry Smukler alimtaja Labrie kuwa 'muongo wa kupindukia' alipotoa hukumu hiyo ya mwaka mmoja gerezani.BBC



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: