SECONDARY SCHOOL
Sehemu Ya 13
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
"eti bosi kumbe kuna nafasi za kazi?? nipe basi bosi"
"we mtoto acha mdomo mchafu..... afandeeee? afandee? we afande?"
"abee bosi?"
"toa hizi taka taka hapa?"
"sawa afande"
Daaahh tulianza kushikwa tanganyika jeki na yule afande wa kike
"afande utatuumiza bwana"
"tokeniiiii"
Nikaona hapana hii sio haki kabisa
"afande niachie haraka"
"unasemaje we mtoto?"
SONGA NAYOOOO
Nilianza kua mjeuri maana najua wakisikia tu kua mimi ndio part of this watachanganyikiwa mno. Sasa tulikua tumeshikwa tanganyika jeki huku suruali yangu ikiwa inajikunja jikunja kwa kushikwa na afande huyo.
"afande utatuumiza"
"sasa si mtoke?"
"lakini hii ni haki yetu kuomba kazi kama jinsi nyinyi mlivyokuja kuomba kazi hapa, hivyo ninachokiomba mimi naomba mtuache"
"tuwaache mkiwa kama nani?"
"ok sawa tuitieni meneja muajiri"
"meneja muajiri au boss mkuuu anaumwa kwaio hayupo"
"basi tunamsubiri hapa hapa"
"afu we mtoto wewe ndio kiburi si ndio?"
"hapana ila ni haki yetu kupata kazi"
Nikaona ngoja nimtoe chemba huyo meneja ili niangalie kwenye upande wa rushwa
"boss hebu tuongee kiutu uzima basi"
"utaongea nini wewe mtoto?"
"we si uje tu"
Nilitoka nae yule meneja kwa pembeni kisha nikaanza kuongea nae... huju wale vijana wanne wanao omba kazi nikawa kama tegemezi lao, maana wao walionekana kua waoga mno.
"sasa boss? hebu tuelewane kwanza kiutu uzima sawa?"
"hebu sema wacha kuzunguka zungukaa"
"ok sasa boss vp bwana sisi tunataka kazi ndugu yangu. na kama vp tutaangaliana kwenye upande wa maji ya kunywa au unasemaje?"
"we nani kakuambia mi nataka rushwa?"
Alikua akiongea huku akiangalia huku na kule kama kuna watu watamuona kisha akaniambia kua
"hebu njoo huku coz unaonekana una akili sana we dogo mmhhh?"
"ndio mzee nina shida na kazi"
"ok hebu sema sasa"
"sasa boss? mimi naweza kutoa chochote kile ili nipate kazi"
"ok sawa kijana ila unaweza kutoa chochote kile?"
"lakini nafasi zipo boss?"
"aaa tena zipo nafasi 6 za nguvu"
"sasa mbona ulikua unatubania?"
"aaaa si unajua maisha haya dogo langu?"
"ok kwaio sasa utatuchaji shing ngapi?"
"kwa nyie toeni mia na hamsini kila mmoja tu"
"aaaa kaka sasa sisi ndio tunatafuta kazi afu unatupiga pesa yote hio?"
"ok poa kwakua ni madogo zangu toeni ata laki laki kila mmoja basi"
"ok atilist hio nitajitaidi hata kuwalipia na hawa ndugu zangu"
"heeee unawalipia na wale wengine?"
"ndio, ni ndugu zangu niliwaacha hapo nje"
Niliitoa walet yangu na kuesabu shilingi laki tatu peee... mpaka mwenyewe alishtuka
"heeeeee we dogo?? umekuja kuomba kaaaaaziiiii au umekuja kutuinjoi tu?"
"kwanini boss?"
"haaaaaa yaani walet imevimba kuliko boss?"
"we shika hiii laki 4 zako afu utandai laki 1 kwa ajili yangu"
"aaaa dogoooo pesa si hizo umerudisha kwenye walet? tena walet yenyewe haijastuka hata kidogo kama imetolewa pesa"
"sikia boss unajua mimi ndio nayaanza maisha hivyo hapa nakwenda kununua kitanda na kupangisha chumba kimoja afu sina hata chombo.. yaani kifupi ndio nayaanza maisha"
"ok kwaio lini utanimaliza hio laki yangu?"
"aaaaa kaka tufanye mshahara kaka"
"ila usiponilioa ni nje"
"haina shida kaka"
Basi broo alituchukua na kutuingiza ndani kwa wote. kisha akaanza kutuuliza maswali kabla ya intaviu..
"haya hebu nione vyeti vyenu"
Sasa hapo mimi sikua na vyeti bali nilikua na docoment za kusaini tu hivyo mimi nikawa nimewekwa pending kwanza kisha akaniita mimi peke yangu
"sasa wewe vyeti vyako vipi?"
"bosi nilisahau kuvibeba nikajua ndio vyenyewe kumbe ni mikaratasi mingine tu"
"sasa itakuaje?"
"labda kesho boss?"
"mh mh apana mi nataka tumalize leo leo"
"basi bosi nifanye kama umeona vyeti vyangu alafu nitakuongezea kidogo"
"dogo tafadhali sana kwanza pesa yako hujaimalizia cha pili vyeti huna je nitaelewekaje kwa mkuu wangu endapo atadai vyeti vyako afu nikamuambia sina?"
"lakini boss?"
"hakuna cha lakini mi nataka vyeti vyako......Ehee nanyie vp si nimewaambia mkalete barua za wazamini na barua za viongozi wenu wa mtaa na paspoti nne"
Nikaona sasa hii ni mateso yaliokisiri mno Yaani hongo utoe bado uhangaikie mabarua???? aaa yani hii sio haki kabisa inayoendelea ndani ya kampuni hiii...
Sasa mimi nikamjibu boss badala ya hawa vijana ambao wapo wavulana wawili na wasichana wawili
"lakini boss? mbona hatuioni faida ya hongo?"
"kivipi?"
"sisi tumetoa hongo ili vingine ufanye wewe, sasa iweje uanze kutupa hizo kazi za kuzunguka kwa watendaji mabalozii sasa basi tupe pesa yetu ili tufatilie hivyo vitu"
"kwahio hivyo vyeti na paspot utaleta huleti?"
"kwa upande wangu mimi sileti"
"basi naomba utoke nje ya ule mlango paleee.. na nyie nataka kesho mulete hivyo vigezo kisha niwafanyie intaviu sawa?"
Wakamjibu boss kua
"lakini boss? sisi ni wageni ambao hata mabalozi wetu hatuwajui na hata huyo mzamuni tutamtoa wapi?"
"okeeee na mimi hapo sina cha kuwaseidia kwani hapo ni sheria ichukue mkondo wake"
"kwaio boss? kazi tunayo au?"
"kiukweli hata pesa zenu sizitaki"
"ok kwai ndio umekataa kutupa kazi sio?"
"ebu tokeni mbele ya macho yangu na pesa yenu siwapi afu hamnipeleki popote tokeniiiiii"
tulitoka pale kuelekea pale alipo sesi ambae ndio secretary wa kampuni hiiii.
"dada samaani naomba simu yako mara moja"
"heeeee ulinipa pesa ya vocha?"
"tafadhali sana naomba kwa mara moja tu"
"sitakiiii heee kwani lazima?"
"ok shika hii elfu kumi"
"yes ayo ndio mambo sasa"
Mara meneja akaja mpaka pale tulipo
"nyie bado hamjaondoka tuuu?"
"aiseee ndugu tuondoke zetu tusije zua balaa... twendeni tukajaribu kwenye kampuni nyingine"
"subiri kwanza niongee na mtu fulani"
Tulikua tukiongea sisi tuliokua tuna shida ya kazi, kwani wenzangu walikua wanaogopa sana karibia watetemeke... afu nikicheki kuna watoto wazuri nao wanataka kazi...
"we kijana? unataka kumpigia nani?"
"hapana boss bali nataka nimjulishe mama angu kua nimekosa kazi"
"yaani katika mapumbavu we ni namba moja kweli wewe...hebu nipisheni mimi mschiuuu"
Nilipewa simu na yule sesi huku akiniangalia jnsi ninavyofanya
"mmhhh simu yako siwezi kuitumia hebu andika hizi namba mwenyewe"
Nikampa simu yake kisha nikaanza kumtajia namba moja baada ya nyingine, huku meneja akiangalia tukio zima jibsi linavyofanyika
"Enhe taja hizo namba zako"
"ok ni 0714"
"Enhee?"
"4194"
"heeee mbona kama namba ya boss wetu hio?"
"kwani zimeisha dada?"
"ok endelea"
"mwisho ni 87 tu"
"si nilikuambia kua hii ni namba za boss wetu...we umezitoa wapi?"
"we piga tuuu shida ni nini?"
Alikua anasita kupiga Nikampokonya ile simu na kuipiga tena niliweka laudi spika.... huku meneja akiwa anazunguka zunguka tu huku na kule.
"haloo sesi? ivi mwanangu si kafika huko?"
"hapana hapa huongei na sesi bali unaongea na kijana sharbiny hapa.... sasa boss? huku kuna vijana wanataka kazi je? kuna nafasi au hakuna?"
"we unaongelea nini? mbona sikuelewi sheby?"
"nakuuliza boss huku kuna nafasi au hakuna?"
"zipo nafasi kama sita hivi ila hazijapata watu bado"
"sasa hapa kuna vijana wanahitaji kazi je? wapewe kazi ama?"
"okee mwambie kevin awakague vyeti vyao afu awafanyie intaviu then awape kazi"
"ok na je kuna rushwa yeyote inatakiwa kupokelewa?"
"hapana lakini ni kwanini unauliza hivyo sheby?"
"ok boss asante na natumai tutapata kazi... nakutakia mchana mwema baibai"
Nilikata simu kisha nikamgeukia meneja.... huku sesi akishangaa kujibiwa vizuri na boss wao
"lakini mbona umeongea vizuri na boss?"
"hio haikuusu.... sasa kevin naona umesikia kila kitu afu cha kwanza naomba unipe pesa yangu"
"pesa sikupi na nitampigia simu boss na kumuambia kua hawa watu hawana vigezo kamilia vya kufanya kazi na sisi"
"kweli?"
"afu we kijana sijui umeibia wapi namba ya boss wetu pumbavu wewe"
"sawa we tukana tu"
"afandeeee?"
"beeeeee"
"njooo piga hawa watu"
Sasa afande ile kuja tu mara simu ikaita kwa sesi
"haloo boss?"
"Eti sesi kuna tatizo gani?"
"mbona hakuna kitu boss"
"mumemuona mtoto wangu wa pekee? na ndio bosi wenu huyo maana hana tofauti na mimi wala baba yake"
"lakini nadhani bado hajafika huyo mtoto wako"
"tayari mbona keshafika, au mumemdharau?"
"hapana boss hatuwezi mzarau boss"
"sasa mbona hamjui?"
"kwa kwa......kwa ...kwa kwani ni yupi boss?"
"si huyo nilieongea nae kupitia simu yako"
"yesu wangu"
Sesi aliiponya hadi simu na kuidondosha chini huku akiwa kabaki mdomo wazi na kutoa macho
Kevin akamuuliza sesi
"sesi vp nani ulikua unaongea nae?"
"boss"
"kasemaje kwani?"
"boss wako?"
"nani boss wangu?"
Akanyoosha kidole kuashiria ni mimi
"kivipi sesi?"
"ndio mtoto wa boss huyo"
"whaaat?"
Usikose kufatilia juu ya maamuzi nitakayo yachukua juu ya wafanyakazi hawa
Press like ujioneee nitakavyofukuza mmoja baada ya mwingine
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment