MATOKEO MECHI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA


Oktoba 21, 20115  
VfL Wolfsburg 2-0 PSV
CSKA Moscow 1-1 Manchester United
Atletico de Madrid 4-0 FC Astana
Galatasaray 2-1 Benfica
Paris Saint-Germain 0-0 Real Madrid
Juventus 0-0 Borussia Monchengladbach
Malmo FF 1-0 Shakhtar Donetsk
Manchester City 2-1 Sevilla
Oktoba 20, 2015  
FC Porto 2-0 Maccabi Tel Aviv
Dynamo Kyiv 0-0 Chelsea
Valencia CF 2-1 KAA Gent
Zenit St Petersburg 3-1 Lyon
Bayer 04 Leverkusen 4-4 Roma
BATE Borisov 0-2 Barcelona
Arsenal 2-0 FC Bayern Munchen
Dinamo Zagreb 0-1 Olympiakos
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akitafuta maarifa ya kumtoka kiungo wa PSG, Blaise Matuidi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MANCHESTER United imepata sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji CSKA Moscow Uwanja wa Arena Khimki katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Seydou Doumbia alianza kuifungia CSKA dakika ya 15 kabla ya Anthony Martial kuwasawazishia Mashetani Wekundu dakika ya 65.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, VfL Wolfsburg imeshinda 2-0 dhidi ya PSV, mabao ya Bas Dost dakika ya 46 na Max Kruse dakika ya 57 Uwanja wa Volkswagen Arena.
Real Madrid imelazimisha sare ya bila kufungana na Paris Saint-Germain Uwanja wa Parc des Princes, Paris katika mchezo wa Kundi A. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Malmo FF imeshinda 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk, bao pekee la Markus Rosenberg dakika ya 17 Uwanja wa Swedbank.
Atletico Madrid imeshinda 4-0 dhidi ya FC Astana katika mchezo wa Kundi C, mabao ya Saul Niguez dakika ya 23, Jackson Martinez dakika ya 29, Oliver Torres Munoz dakika ya 63 na Denis Dedechko aliyejifunga dakika ya 89 Uwanja wa Vicente Calderon.
Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial akienda chini baada ya kukwatuliwa na mabeki wa CSKA Moscow  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mchezo mwingine wa kundi hilo, Galatasaray imeshinda 2-1 dhidi ya Benfica, mabao yake yakifungwa na Selcuk Inan kwa penalti dakika ya 19 na Lukas Podolski dakika ya 33, baada ya wageni kutangulia kwa bao la Nicolas Gaitan dakika ya pili Uwanja wa Turk Telekom Arena.
Juventus imelazimishwa sare ya 0-0 Borussia Monchengladbach katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Juventus, wakati Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Sevilla katika mchezo mwingine wa kundi hilo Uwanja wa Etihad.
Adil Rami alijifunga dakika ya 36 kuipatia Man City bao la kwanza kabla ya Yevhen Konoplyanka kusawazisha dakikaa ya 30 na Kevin De Bruyne kuwafungia bao la ushindi wenyeji dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya dakika 90.
Mechi za Jumanne, Arsenal iliichapa 2-0 FC Bayern Munich katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Emirates, London, mabao ya Olivier Giroud dakika ya 77 na Mesut Ozil dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Olympiacos ya Ugiriki ilishinda 1-0 ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb, bao pekee la Brown Ideye dakika ya 79 Uwanja wa Maksimir.
Mabao mawili ya kipindi cha pili ya Ivan Rakitic dakika ya 48 na 64, yaliwapa mabingwa watetezi, Barcelona ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya BATE Borisov Uwanja wa Borisov Arena katika mchezo wa Kundi E.
Kevin De Bruyne akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Man City PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Barca inaendelea kuwa kileleni mwa kundi hilo, kwa kufikisha pointi saba, tatu zaidi ya Bayer 04 Leverkusen iliyolazimishwa sare ya 4-4 na Roma jana.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia mabao mawili Bayer Leverkusen, kwanza kwa penalti dakika ya nne na lingine dakika ya 19, mabao mengine yakifungwa na Kevin Kampl dakika ya 84 na Admir Mehmedi dakika ya 86.
Mabao ya Roma yalifungwa na Daniele De Rossi dakika ya 29 na 38, Miralem Pjanic dakika ya 54 na Iago Falque dakika ya 73 Uwanja wa BayArena.
Chelsea imepata sare ya 0-0 ugenini mbele ya Dynamo Kyiv Uwanja wa Kiev Olympic katika mchezo wa Kundi G.

Mario Mandzukic (katikati) akipambana na wachezaji wa Monchengladbach, Xhaka (kushoto) na Dominguez  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Porto walipanda kileleni kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, mabao ya Vincent Aboubakar dakika ya 37 na Yacine Brahimi dakika ya 41 Uwanja wa Estadio do Dragao.
Valencia CF ilishinda 2-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Kundi H, mabao yake yakifungwa na Sofiane Feghouli dakika ya 15 na Stefan Mitrovic aliyejifunga dakika ya 72, wakati bao la wageni lilifungwa na Thomas Foket dakika ya 40 Uwanja wa Mestalla.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Zenit St Petersburg iliichapa 3-1 Lyon, mabao yake yakifungwa na Artem Dzyuba dakika ya pili, Givanildo Vieira de Souza dakika ya 56 na Danny Miguel Alves Gomes dakika ya 82, huku bao pekee la wapinzani wao likifungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 49 Uwanja wa Petrovski.



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: