- LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
1545 Chelsea v Liverpool
1800 Crystal Palace v Man United
1800 Man City v Norwich
1800 Newcastle v Stoke
1800 Swansea v Arsenal
1800 Watford v West Ham
1800 West Brom v Leicester
++++++++++++++++++++++++++++
LEO zipo Mechi 7 za Ligi Kuu England lakini Bigi Mechi ni ile ya kwanza kabisa hii Leo huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Liverpool ikizikutanisha Timu ambazo ziko Nafasi ya 9 na nyingine ya 15 huku wingu kubwa likitanda kuhusu hatima ya Jose Mourinho.
Licha ya mwenyewe Mourinho kusisitiza hana wasiwasi na kibarua chake kama Meneja wa Mabingwa Watetezi Chelsea lakini mwanzo mbovu uliowafanya wawe Nafasi ya 15 ni mkosi mkubwa.
Wakiwa wameshinda Mechi 3 tu za Ligi kati ya 10, wakitupwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Man City, Mourinho Jana alisisitiza: “Sina wasiwasi na kazi yangu. Situmii hata Sekunde 1 ya Siku yangu kufikiria hilo!”
Hata hivyo, ripoti za Mitaani ni kwamba Mourinho atafukuzwa kazi ikiwa Chelsea itafungwa na Liverpool hii Leo.
Hili litakuwa pigo kubwa kwake ingawa linaweza kumletea mavuno makubwa kwani Mwezi Agosti alisaini Mkataba mpya wa nyongeza ya Miaka Minne hadi Juni 2019.
Lakini kwa Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, kutimua Meneja kutokana na wasiwasi wa kutotinga 4 Bora ili kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu unaofuata si kitu kikubwa kwani ashafafanya hivyo mara nyingi tu.
+++++++++++++++++++++++
MOURINHO v KLOPP:
-Katika Mechi 4 walizokutana, Mourinho amembwaga Jurgen Klopp mara 1 tu na kupata Sare 1 na kufungwa mara 2, zote zikiwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2012/13 ambapo Borussia Dortmund iliitoa Real Madrid kwa Jumla ya Mabao 4-3 katika Nusu Fainali.
+++++++++++++++++++++++
Hali za Wachezaji
Chelsea watampima Straika wao Diego Costa kama yuko fiti baada ya kuumia mbavu walipofungwa na Stoke City kwenye Capital One Cup Jumanne iliyopita.
Mchezaji mwingine wa Chelsea atakaepimwa ni Pedro lakini Nemanja Matic anarejea baada ya Kifungo cha Mechi 1 wakati Majeruhi ni Branislav Ivanovic na Kipa Thibaut Courtois.
Kwa Liverpool, James Milner anarejea baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi 1 huku Majeruhi ni Daniel Sturridge na Kolo Toure.
Habari njema kwa Liverpool ni kuwa fiti tena kwa Straika wao Christian Benteke aliekuwa na tatizo la Goti.
Uso kwa Uso
-Chelsea hawajafungwa na Liverpool katika Mechi zao 8 zilizopita za Ligi na Vikombw. (Ushindi 4, Sare 4).
-Liverpool walipata ushindi mara 3 mfululizo Uwanjani Stamford Bridge Mwaka 2011 lakini tangu wakati huo hawajashinda tena.
Refa
Ni Mark Clattenburg akisaidiwa na S. Child na S. Beck huku Refa wa Akiba ni Lee Mason.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Novemba 1
1630 Everton v Sunderland
1900 Southampton v Bournemouth
Jumatatu Novemba 2
2300 Tottenham v Aston Villa
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
0 comments:
Post a Comment