Mazoezi Ya Pelvic Floor Ni Nini?
Mazoezi ya pelvic floor ni mazoezi yanayofanywa ili kuikomaza misuli inayoshikilia kibofu cha mkojo na sehemu ya haja kubwa. Misuli hii (pelvic muscles) huanzia kwenye kinena na kuzunguka hadi inapoishia mifupa ya uti wa mgongo na ipo katikati ya miguu. Hii ndiyo misuli inayokusaidia uweze kudhibiti mkojo, uamue kukojoa au kuubana usitoke. Mazoezi haya yanalingana sana na mazoezi ya Kegel na yana malengo yanayolingana. Ni mazoezi muhimu kwa wanawake wanaotaka kukaza misuli ya uke au wanaotaka uke kuwa mdogo (unaobana). Mara nyingine mazoezi ya misuli ya pelvic floor huitwa mazoezi ya Kegel.
Faida Za Mazoezi Ya Kukaza Misuli Ya Uke
Misuli ya Pelvic floor hupungua nguvu yake kadri umri wa mtu unavyoongezeka. Misuli hii pia hulegea kadri mwanamke anavyozaa zaidi. Misuli ikipungua nguvu au ikilegea, husababisha mtu atokwe na mkojo bila kukusudia. Kwa wanawake, misuli hii ikilegea husababisha ashindwe kufaidi tendo la tendo kwa sababu sehemu zake nyeti huwa pana, hali ambayo pia husababisha ashindwe kumridhisha mwenzi wake. Hali hii huweza kusababisha mwanamme aanze michepuko. Kwa hiyo faida za mazoezi haya ni kumfanya mtu asipatwe na hali ya kutokwa na mkojo bila kukususudia na aweze kufaidi tendo la ndoa kwa kukaza misuli yake ya uke na kufanya uke kuwa mdogo, au kwa maneno mengine, unaobana .
Mazoezi Ya Pelvic Floor Ni Kwa Ajili Ya Nani?
Mazoezi haya ni kwa ajili ya jinsia zote. Mwanamke anapokuwa na mimba ni vizuri aanze kufanya mazoezi haya ili kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la kutokwa na mkoja baada ya kuzaa. Baada ya uzazi mazoezi haya hukaza misuli ya uke iliyolegea kwa uzazi na kumfanya mwanamke na mwenzi wake wasikie zaidi raha ya tendo la ndoa. Mazoezi haya pia huwasidia wanaume wenye matatizo ya jogoo kushindwa kuwika au wale wanaotokwa na mkojo bila ridhaa yao.
Jinsi Ya kufanya Mazoezi Ya Kukaza Misuli Ya Uke
Kuna mazoezi ya namna nyingi na kuna vifaa vingi vilivyotengenezwa ili kumsaidia mtu kufanya mazoezi haya, lakini yote yana lengo moja kuu – kukomaza misuli inayozunguka pelvis. Moja ya mazoezi mazuri ni kama ilivyoonyeshwa kwenye video hii hapa chini. Panga ratiba yako nzuri ya mazoezi ili uweze kunufaika na mazoezi haya. Ukiyafanya vizuri, kwa hakika utapata faida zilizoorodheshwa hapo juu.
Ili kujua kwa undani tatizo la uchi kulegea au uchi kuwa mpana, rejea ukurasa wa “Uchi Kulegea” na kujua kwa undani tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni, rejea “Kuwahi Kufika Kileleni.”
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment