Jogoo Kushindwa Kuwika – Erectile Dysfunction

 
jogoo hawiki

Tatizo La Jogoo Kuwika – Erectile Dsysfunction


Kuna tatizo ambalo wengi huwa tunaliita ukosefu wa nguvu za kiume. Neno hili kama linavyotumika mimi naliona ni pana mno na halielezei hasa ni kitu gani kinamaanishwa kwani kuna matatizo lukuki ambayo yote yapo katika kundi la ukosefu wa nguvu za kiume. Leo tutazame tatizo ambalo limeliita tatizo la jogoo kushindwa kuwika au jongoo kushindwa kupanda mtungi. Kwanza tutazame tatizo hili lipoje.

 Nini Maana Ya Jogoo kushindwa Kuwika

Hii ni hali inayomtokea mwanamme ambapo anakuwa na hamu ya upungufu wa nguvu za kiumekufanya tendo la ndoa lakini uume wake au hausimami kabisa, kukosa kusimama kikamilifu au kusimama kikamilifu kwa muda mfupi sana hivyo kukosa nguvu ya kufanya tendo lililokusudiwa. Nusu wa wanaume hupata tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40, idadi ikiongezeka kwa wanaume wenye umri mkubwa zaidi, kwa mfano asilimia 70 ya wanaume wenye miaka 70 huwa na tatizo hili. Ifahamike kwamba kila mmoja wetu huweza kupata tatizo hili kwa muda fulani kutokana na vitu kama uchovu, kupata kilevi, kutoelewana na mwenzi n.k. Tunasema mwanamme ana tatizo hili pale hali hii inapoendelea kwa kipindi kirefu, kwa mfano hali hii ikitokea kwa mwezi mzima mfulululizo.

 Sababu Za Tatizo La Jogoo Kushindwa Kuwika

Kuna mengi yamesemwa kuhusu chanzo cha tatizo hili. Imani iliyoenea ni kwamba tabia ya vijana kujichua (kupiga nyeto) ndiyo inayosababisha tatizo hili. Mimi sijaona pahali wataalamu waliposema hivyo, nafikiri si kweli ukizingatia kwamba wataalamu wamekuwa wakiwashauri vijana kufanya hivyo kuliko kwenda seheme za machangudoa pale wanapozidiwa. Ukizingatia kwamba tendo la uume kusimama linahusisha ubongo, homoni, misuli na mishipa ya damu, tatizo katika hayo ndilo linaloweza kusababisha jongoo ashindwe kupanda mtungi. Baadhi ya sababu zinapelekea uume kutosimama au uume kukosa nguvu ni:
  •  Magonjwa ya moyo
  •  Unene wa kupindukia
  •  Ugonjwa wa kisukari
  •  Uvutaji wa sigara
  •  Utumiaji wa pombe

Madhara Ya Tatizo La Jongoo Kushindwa Kupanda Mtungi


Kuna madhara mengi yanayotokana na tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi. Mwanamme anayepatwa na tatizo hili hushindwa kumridhisha mwenzi wake na hali hii huweza uume kushindwa kusimamakusababisha matatizo makubwa katika mahusiano ya kimapenzi au katika ndoa. Hali hii hupelekea mwanamme huyu kuanza kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo, huanza kukosa kujiamini na kujiona ana mapungufu. Tatizo hili pia linasababisha mwanamme huyu ashindwe kumpa ujauzito mkewe.

Tiba Za Tatizo La Jogoo Kushindwa Kuwika

Ifahamike kwamba uume kusimama maana yake damu kuingia katika kiungo hicho, hivyo tiba ya uume kutosimama ni kutafuta njia ya kufanya damu ifike kwenye kiungo hicho kwa kiasi kinachotakiwa. Hii ni pamoja na kuondoa matatizo ya moyo, kupunguza unene, kupunguza cholesterol na kutumia dawa za kufungua njia za mishipa ya damu.

dawa ya nguvu za kiume

Njia nyingi zinatumika kuyafanya hayo hapo juu. Wenzetu hufanya hata upasuaji wa uume lakini kwetu sisi hilo bado sana. Kuna pampu zinauzwa kwa kusaidia damu ielekee na kujaza mishipa ya damu inayozunguka uume lakini hizi zinasaidia kwa muda mfupi. Dawa nyingine ambazo watu hutumia ni pamoja na viagra, Cialis na Levitra.
Ipo mimea mingi iliyothibitishwa kuwa inasaidia au kuponya kabisa tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na makampuni mbalimbali yamekuwa yakitengeneza dawa kutokana na mimea hiyo. Dawa hizo hupatikana kama vidonge au unga ambao hutumiwa kwa kunywewa kama chai au kahawa. Mimea maarufu iliyothibishwa ni pamoja na epimedium, ginseng na rhodiola rosea.
Mmea wa epimedium tutauzungumzia kwa kina katika ukurasa tofauti baada ya wataalamu kubaini kuwa ukikamuliwa hutoa icariin ambayo imetumika kutengeneza dawa ya kusaidia kuondoa tatizo la uume kushindwa kusimama kikamilifu. Dawa hii kuitwa Horny Goat weed na inatumika na watu wengi sana duniani.
Katika kurasa nyingine tofauti tutajadili matatizo ya Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume, tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake na tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema kwa wanaume.
Jee, una tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na ungependa kupata maelezo ya kina zaidi au kusaidiwa kupata dawa za kutumia? Usisite kuwasiliana nasi.


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment