NAIBU
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana amepigwa
chini katika kura za maoni za ubunge wa viti maalumu kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe.
Wajumbe
wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa chama hicho, mkoania
Njombe walimchagua Dk Suzan Kolimba na Neema Mgaya kuingia katika kundi
la washindi wawili wa ubunge wa viti maalumu kutoka kila mkoa nchini
katika kura za maoni zilizofanyika jana, mjini Njombe.
Wakati
Dk Kolimba alikuwa mshindi wa kwanza kwa kupata kura 252, Mgaya alikuwa
wa pili akipata kura 213 huku Dk Chana akiambaulia kura 164 zilizofanya
awe mshindi wa tatu, ushindi ambao haumpeleki tena bungeni kuwakilisha
wanawake wa mkoa huo.
Mwingine
aliyeanguka katika kura hizo za maoni ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje,
Rosemary Sitaki aliyeambulia kura 38 huku Erika Sanga akipata kura 107
na Magret Kyando akiambulia kura tano.