WALIMU VIJIJINI WILAYANI LUDEWA MKOA WA NJOMBE WAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU




Hii ni nyumba ya mwakimu mkuu wa shule ya msingi Masimavalafu

Milango na madirisha ya nyumba ya mwalimu

Huo ni mkeka ukiwa kama mlango katika nyumba hii ya mwalimu,



choo cha nyumba ya mwalimu mkuu wa shule

choo cha nyumba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi masimavalafu katika kata ya Ibumi.

 Walimu wa shule ya msingi masimavalafu katika kata ya Ibumi  wilayani Ludewa mkoani Njombe wameilalamikia serikali ya kijiji hicho kwa kutoonyesha ushirikiano katika shughuli zinazotakiwa kusimamiwa na viongozi wa kijiji hicho pamoja na serikali ya kijiji kwa ujumla.

Ludewa ,,  Walimu wa shule ya msingi masimavalafu katika kata ya Ibumi  wilayani Ludewa mkoani Njombe wameilalamikia serikali ya kijiji hicho kwa kutoonyesha ushirikiano katika shughuli zinazotakiwa kusimamiwa na viongozi wa kijiji hicho pamoja na serikali ya kijiji kwa ujumla.

Wakizungumza na www.maikoluoga.blogsport.com hivikaribuni walimu wa shule hiyo walisema kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili walimu hao pamoja na wanafunzi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa choo katika nyumba ya mwalimu mkuu hali inayoonekana  kuwa ni changamoto kubwa kwa mwalimu huyo hasa mazingira ya kufanya kazi katika shule hiyo.

Aidha walimu hao waliitaja changamoto nyingine kuwa ni nyumba ya mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo kutokuwa na milango ya nyumba pamoja na madirisha kwa takribani miezi mitatu mpaka sasa tangu milango hiyo iharibike ambapo kwa sasa wameweka mkeka kama kizuizi huku wakisema wamejaribu kupeleka jambo hilo katika uongozi wa serikali ya kijiji hicho lakini hakuna majibu wala utekelezaji wa jambo hilo ambapo walimu hao wanazidi kuwa na mazingira magumu licha ya kuendelea kufanya kazi ya kufundisha wanafunzi kilasiku.

Waliongeza kuwa wanampongeza diwani wa kata ya Ibumi kupitia chama cha mapinduzi ccm mh, Edward Haule kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la ludewa Mh, Deo Filikunjombe ambao kwa pamoja wanamaliza muda wao wa uongozi kwa kipindi cha miaka mitano sasa kwakupeleka mifuko ya sment na bati kwaajili ya ujenzi wa vyoo vitatu vya nyumba za walimu lakini vifaa hivyo hadi leo havijafanyiwa kazi kutokana na uzembe wa uongozi wa kijiji hicho cha masimavalafu.

Alipotafutwa mwenyekiti wa kijiji cha masimavalafu pamoja na mtendaji wa kijiji hicho aliye julikana kwa jina la Majaliwa Komba walikwepa kulizungumzia hilo kwa madai kuwa hawana lolote la kuzungumzia kisa ni kipindi cha uchaguzi wakati huo walimu wa shule yao wanaendelea kuteseka katika mazigira magumu hivyo kwa kauli hiyo inaonesha wazi kuwa uongozi wa kijiji hicho umekubaliana na mateso makubwa wanayokumbananayo walimu wao.

Shule ya msingi masimavalafu inawalimu wawili kwa zaidi ya miaka nane hadi sasa haliinayosababisha kushuka kwa kiwango cha elimu katika shule hiyo kwakuwa inaupungufu wa walimu wapo wawili na wote ni walimu wa jinsi moja ya kiume.

Vyoo vya nyumba za walimu vipo katika hali mbaya saana kwakuwa vimeanza kubomoka na uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wananchi wanazidi kulitazama jambo hilo bila kulitafutia mbinu za kulitatua.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: