Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzomewa nawananchi wa jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.Inadaiwa kuwa Mbunge huyo alipanda jukwaani kwa lengo la kuomba kura ikiwa ni kutaka kugombea tena jimbo hilo la Muleba, jambo ambalo lilizua mzozo na kujikuta akiaibika mbele ya Komradi Kinana.Inadaiwa kuwa Tibaijuka alisema “Anayetaka kusikiliza abaki na asiyetaka aondoke,” ambapo Mkuu wa Wilaya, Francis Isack, ilibidi kuchukua jukumu la kuwanyamazisha wananchi hao ambao walianzisha fujo.Inadaiwa kuwa baada ya kauli hiyo wananchi walitulia na kuruhusu Profesa Tibaijuka, kupanda na kuhutubia kwa muda ambapo bila kutegemea wananchi walirushiwa komboratena jambo ambalo huenda likawa limetafsiriwa vibaya na wananchi.“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibumkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema.“Mimi sitafuti kazi na wala sina njaa… na kama hela ya kula ninayo. Mimi sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone atawasaidia vipi,”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment