Mashabiki wa Yanga jana walifurika uwanja wa Karume kushuhudia mazoezi ya timu yao, lakini walipomuona Ramadhan Singano ‘Messi’ akiingia kwenye Ofisi za TFF kwa ajili ya kikao cha kujadili utata wa mkataba wake na klabu ya Simba. Tofauti walimshangalia na baadaye kuchangishana pesa walizompatia wakijigamba kuwa Simba haina hela za kumpa hivyo ajiunge na Yanga.
Ulikuwa utani wa jadi lakini kitendo hicho kimetafsiriwa tofauti na wadau wengi na kumezuka tetesi kuwa kiungo huyo mshambaliaji amejiunga na mabingwa wa Tanzania bara, Young Africans.Kutokana na taarifa hizo, Singano amekiri kupokea simu nyingi zikimuuliza kama kweli kajiunga na Yanga lakini amekanusha uvumi huo.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook unaokwenda kwa jina la Ramadhan Singano Messi amekanusha taarifa hizo na ameandika hivi “Nimepokea simu nyingI sana wakiwa wananiuliza kama ni kweli nimejiunga Yanga ila mimi nasema siyo kweli na sina mpango huo mimi bado naipenda simba”
Kwa jicho la ziada hapa mimi naona kwamba Singano kutetea haki yake ya kimkataba sio kwamba anaichukia Simba wala timu nyingine zisichukue advantage ya matatizo yake na Simba kutaka kumchukua kiurahisi. Kinachofanyika ni kutetea haki ya msingi kwenye mkataba wake na sio kwamba anaichukia Simba. Anaweza kumaliza matatizo na matakwa yake kwenye mkataba yakazingatiwa anakubali kusaini tena na Simba. Ishu sio kuichukia Simba bali ni kutetea haki yake ya msingi kwenye mkataba wake na Simba
0 comments:
Post a Comment