Mjumbe UN ajiondoa Mgogoro wa Burundi


Baadhi ya wananchi katika Maandamani nchini Burundi.
Baadhi ya wananchi katika Maandamani nchini Burundi.
Umoja wa mataifa umesema mjumbe wake maalum katika eneo la maziwa makuu hataendelea tena kuwa mpatanishi katika mzozo wa Burundi.
Msemaji wa umoja huo Vladimir Monteiro amesema mjumbe huyo Said Djinnit amejiondoa kutoka kwa harakati hiyo iliyokuwa inatafuta mwafaka kati ya vyama vya upinzani na kile kinachotawala cha rais Pierre Nkurunziza anayekabiliwa na shinikizo za maandamano  kupinga hatua yake ya kuwania muhula mwengine kama rais wa nchi hiyo.
Hakuna sababu zozote zilizotolewa kuhusu kujiondoa kwa bwana Djinnit lakini awali makundi ya upinzani yalikuwa yamedai kuwa afisa huyo alikuwa anaupendelea upande wa serikali madai ambayo hata hivyo anayoyakana.
Licha ya hatua hiyo bwana Djinnit ataendelea kuwa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika nchi za maziwa makuu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: