Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa ujumbe wake wa watu wanane wamenusurika kifo kufuatia ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege kabla ya kutua.
Katika tukio hilo Waziri Membe alikuwa akisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo na kusisitiza kuwa wamepona kwa rehema za Mwenyezi Mungu.
Katika ajali hiyo idaiwa kuwa watu wa Contol Center walipitiwa suala lililopelekea kutaka kutokea ajali hiyo.
Akizungumzia tukio hilo Membe amesema ana uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali sehemu nyingi duniani na kusisitiza kuwa anajua Mungu yuko upande wake katika safari hii ya uhakika ambayo amesisitiza kuwa ni ya kazi ya Mungu.
Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini Zanzibar na Umoja wa Akimama wa Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano.
Membe ametokea Iringa ambako alikwenda Zanzibar kutafuta udhamini wa chama utakao muwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.
0 comments:
Post a Comment