Bungeni: Uchaguzi mkuu watawala Bajeti 2015/2016


Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akiwasilisha Bajeti ya mwaka 2015/2016.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya akiwasilisha Bajeti ya mwaka 2015/2016.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya  amewasilisha bungeni hotuba ya mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/16 huku  makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/16 ni shilingi trilioni 22, bilioni 495.5
Akiwasilisha Bajeti hiyo  Mkuya amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ukusanyaji  wa mapato yasiyo ya kodi utahusisha faini za mahakamani, faini za usalama barabarani, viingilio katika mbunga za wanyama, vibali vya kuvuna maliasili.
Aidha, mkuya ameainisha maeneo ya ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi ikiwemo matumizi ya utaoji risiti za kielekroniki katika mamlaka ya serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaa na wakala wa serikali.
Kuhusu mapendekezo ya kuongeza tozo amesema serikali imependekeza kuongeza tozo kwenye mafuta ya taa kutoka shilingi 50 kwa lita hadi shilingi mia moja hamsini kwa lita ili kuondoa uchakachuaji wa mafuta’
Amesema kuwa hatua ya kuongeza tozo katika mafuta ya Petroli zinalenga kuongeza mapato ambayo yataelekezwa katika mradi wa usambazaji umeme vijijini.
Akielezea shabaha ya msingi ya bajeti ya mwaka 2015/16 Mhe. Mkuya amesema ni  kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya serikali za mitaa kufikia asilimia 13.1 ya pato la taifa ambapo matumzi ya serikali yanatarajiwa kuwa asilimia 20.6 ya pato la taifa
Kwa upande wa vipaumbele  katika bajeti ya mwaka 2015/16 amevitaja kuwa  ni kugharamia uchaguzi mkuu pamoja na gharama zote za bunge lijalo, kuweka msukumo katika miradi inayoendelea ikiwemo   miradi ya umeme na maji vijijini.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: