SUALA LA DKT MENGI KUTISHIWA KUUAWA LAIBUKA BUNGENI DODOMA

Kambi ya upinzani bungeni imeijua juu serikali kwa kitendo chake cha kushinikiza na kutumia ubabe wa kupitisha sheria ambazo ni kandamizi na zenye kubinya na kua uhuru wa vyombo vya habari hatua ambayo imesema inalenga kuliingiza taifa katika giza na kuondoa kabisa dhana ya uwaziambayo serikali inaihubiri kila mara.Akisoma hotuba ya kambi ya upinzani bungeni katika wizara ya habari utamaduni na michezo Mh Joseph Mbilinyi amesema inashangaza kuona kuwa inataka kujiingiza katika mgogoro waandishi wa habari bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi.Aidha kambi ya upinzani imelaani kitendo cha kuwepo kwa vitisho vya kutaka kuuwawa kwa mmiliki wa kituo cha ITV Dk Reginalid Mengi kwamadai kuwa kituo chake kimekuwa kikitoa habari za uchochezi.Awali akiwasilisha bajeti ya wizara ya habari utamaduni na michezo Mh Dk Fenella Mukangara amesema wizara yake itawasilisha muswada wa sheria ya huduma za habari ambapo ukipita utasaidia kuweka misingi imara katika sekta ya habari.Lazaro Nyalandu ni waziri wa maliasili na utalii ambaye naye amewasilisha bajeti yake nakubainisha mipango mbalimbali yakiwemo namna ya kupambana na ujangili.Kwa upande waziri kivuli wa wizara hiyo mchungaji Peter Msigwa ameitaka serikali kuteketeza shehena ya pembe za ndovu ambazo imezikamata ili kuipunguzia serikali mzigo wagharama wa kutunza pembe hizo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: