LUDEWA NASI TUMO WAANZA KUTENGENEZA FILA

Kikundi cha sanaa kijulikanachokwa jina la IVA YOUTH GROUP kilichoko wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeanza kutengeneza Filamu yao ambayo inamahadhi ya wilaya ya Ludewa ikiwa ni Filamu ya kwanza tokea wilaya hiyo innzishwe.Akiongea na wanahabari wakati wa kurekodi Filamu hiyo katibu wa kikunchi hicho Bw.Leonard Lukuwi alisema IVA YOUTH GROUP ni kikundi pekee kilichosajiriwa na baraza la sanaa la Taifa(BASATA) kunafanya kazi mbalimbali za uelimishaji wa jamii katika wilaya ya Ludewa na knapatikana Ludewa mjiniBw.Lukuwi alisema kuwa kikundi hicho kimekusanya wasanii mbalimbali katika kata na vijiji vya wilaya ya Ludewa nakufikia wasanii 30 ambao wanafanya sanaa mbalimbali na mpaka sasa wanaandaa Filamu ya kwanza ambayo itawatambulisha wanaludewa na tamaduni zao.Alisema kuwa wilaya ya Ludewainawasanii wenye vipaji vikubwalakini wamesahaulika kutokana na kukosa wadau ambao wangeweza kuwaibua na kuitangaza wilaya yao katika Taifa na mataifa mengine ambayo yanafuatilia sanaa za Tanzania.“vipaji vipo Ludewa ila kinachokosekana na ufadhiri kwani mpaka sasa kikundi cha IVA hakina mfadhiri na hakija wahi kupata ufadhiri wa aina yoyote licha ya kuwa ni kikundi kikongwe kilianzishwa mwaka 2008 lakini kimekuwa kikitumiwa na mashirika katika kuielimisha jamii katika mambo mbalimbali na sasa tumeamua kutengeneza filamu hii kwa kujichangisha wasanii wenyeweili tuweze kuinua uchumi wetu ndani ya kundi”,alisema Bw.Lukuwi.Filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi juni mwaka huu ikiwa na wasasii chipukizi ambao kwa mara ya kwanza wataanza kuonekana katika ulimwengu wa Filamu nchini hivyo amewaomba wadau mbalimbali kutoa michango kwanjia ya mpesa katika namba 0752 206242 ili kufanikisha filamu hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: