FILIKUNJOMBE AWEKA HISTORIA LUDEWA


Filikunjombe akikabidhi kitanda cha kujifungulia akina mama katika kijiji cha Lupanga

Filikunjombe akikabidhi kitanda cha kujifungulia katika kijiji cha Mavanga

Filikunjombe akikabidhi saruji na Bati kwa walimu wa shule ya msingi Mfaranyaki Mavanga
Filikunjombe akikabidhi saruji na bati kwa viongozi wa kanisa la Anglikan Lupanga
Filikunjombe akiwapungia mikono wananchi wa mavanga wakati akiwasili kijijini hapo
Filikunjombe akiongea na wananchi wa Lupanga

 Wananchi wa Mavanga walivyompokea Filikunjombe kwa shangwe
Filikunjombe akipiga mndele kijiji cha Mavanga
Wananchi wa Lupanga wakiwa na furaha kwa kumpokea mbunge wao


Filikunjombe akicheza na watoto wa chekechea ya Mundindi



Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo akiongea na wananchi wa Mavanga katika mkutano wa hadhara
Hizi ni moja ya zawadi anazopewa na wananchi wake anapowatembelea vijijini
 Hizi ni moja ya zawadi anazopewa na wananchi wake anapowatembelea vijijini
Filikunjombe akifurahi na wanafunzi wa chekechea Mavanga





Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.DeoFilikunjombe amekuwa ni mbunge wa kwanza katika wilaya ya Ludewa tokea Tanzania kupata uhuru kwa kutimiza ahadi zake kwa wakati ikiwa ni historia ya kwanza kwa wananchi ambao kwa miaka mingi wamekuwa na kiu ya maendeleo bila mafanikio.Hayo yametokea jana katika kata ya Mavanga na Lupanga ambako Mh.Filikunjombe alikuwa akikamirisha kutoa ahadi zake katika sekta mbalimbali lakini kubwa zaidi ni lile la kutoa vitanda vya kujifungulia na darubini ya kupima mgonjwa mbalimbali ikiwa ni siku ya akina mama Duniani ambapo aliazimisha katika kata hizo kwa kutimiza ahadi zake za vitanda hivyo viwili vya kujifungulia akina mama.Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofantyika katika nyakati tofauti katika kata hizo wilayani hapa Mh.Filikunjombe alisema kuwa kutokana na umuhimu wa akina mama Duniani imempasa kununua vitanda hivyo viwili ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 5 kwani wanasiasa waliowengi wamekuwa wakiwasahauwatu hao muhimu ambao ndiyo nguzo ya taifa.Alisema katika nafasi yake ya ubunge amekuwa ni mbunge wakuwatumikia wananchi waliompa ridhaa ya kuwaongoza hivyo amekuwa akitumia kiasi cha fedha yake anayolipwa Mbungeni kwa kuwarudishia wananchi katika manunuzi ya vifaa kama Darubini,vitanda na vinginevyo kwani wananchi wa wilaya ya Ludewa ndiyo wenye mamlaka na pesa yake.‘’sijaanza leo kuyafanya haya ninayoyafanya kwani tokea sijawa mbunge na hata nilipopata ubunge nimeendelea kushirikiana na wananchi wa wilaya yangu katika kuleta maendeleo ili kuibadirisha wilaya yetu hivyo ninachowaomba wananchi ni kuvitunza vifaa hivi ili viweze kutumika katika kizazi kilichopo na kijacho’’,alisema Mh.Filikunjombe.Vitu vingine alivyovitoa kwa wananchi ni pamoja na bati 300 mita 3 geji 28 kanisa la AnglikanMavanga bati 50 na saruji mifuko 50 shule ya msingi Mfaranyaki kata ya Mavanga,rangi ndoo 20 na saruji mifuko 50 shule ya Sekondari ya kata ya Mavanga bati 25,saruji mifuko 25 katika shule ya chekechea mavanga,bati miamoja katika ujenzi wa kituo cha maenndeleokanisa katoliki mavanga.Vingine ni bati sabini katika kanisa katoliki la kinyika kata yaLupanga,Bati miamoja kanisa laAnglikan Lupanga, saruji miamoja na bati miamoja katikashule ya msingi Lupanga kitu ambacho kimevunja rekodi ya wabunge wote waliowahi kuiongoza wilaya ya Ludewa na kufikia kukamilisha ahadi alizozitoa kwa wananchi wa jimbo la Ludewa.Aidha diwani wa kata ya Ludewa mjini Mh.Monica Mchiloaliwataka wananchi wa kata hizo kuunga mkono juhudi za Filikunjombe kwani yote anayoyafanya yapo katika ilani ya chama cha mapinduzi hivyo anatekeleza ilani ya CCM hivyo kina mmoja atafakari yale mazuri ya chama ambayo ni msingi wa maendeleo katika wilaya ya Ludewa.Mh.Mchilo alikili kuwa ahadi za mbunge huyo zimetekelezeka kwa muda muafaka hivyo hiyo ni historia mpya wilayani Ludewa kwani hakuna mbunge ambaye aliwahi kuyafanya hayaambayo yanafanywa na Filikunjombe katika suala zima la uletaji wa maendeleo wilayaniHapa.Mwisho.@habari ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: