WANANCHI WAMTAKA MBUNGE KUTAFUTA MGANGA WA JADI AWASHIKISHE ADABU WANAOFANYA WANAFUNZI WA SHULE MOJA KUFELI

Umewahi kukutana na stori za ishu za wanafunzi kulalamika kwamba shuleni kuna mauzauza?? Kenya imetokea.. watu wakaihusisha na imani za kishirikina moja kwa moja. Mbunge wa Kaloleni,Gunga Mwingailibidi ashangae kidogo wakati ambapo alikaribishwa mgeni rasmi kwenye shughuli ya graduation ya wanafunzi waliomaliza.. basi unaambiwa ombi la wazazi lilikuwa moja tu, wanahitaji Mbunge afanye mpango wa kuwaletea mganga ili kuondoa ushirikina ambao wanahisi upo kwenye shule hiyo. Makamu Mkuu wa Shule hiyo,Richard Charoamesema wanafunzi hawafaulu kabisa mitihani ya kitaifa, wanaamini hiyo inasababishwa na nguvu ya uchawi… lakini Afisa ElimuChigulu Mwarumbanae wazo lake halikuwa mbali na hao waliotangulia, yeye akasema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakisumbuliwa na nguvu za kishirikina na ofisi yake imepokea malalamiko ya aina hiyo mara nyingi. “Mambo yanayoendelea shuleni hapa yanaogofya mno, wasichana wanaanguka hovyo na kuzimia.. wanafunzi wanaanguka mitihani ya kitaifa, tulileta wahubiri wawili lakini hakuna mabadiliko yoyote.. sasa itabidi tulete mtaalamu wa kufukuza mapepo, ninaamini kuna kitu kilizikwa shuleni hapa ili kuzuia wanafunzi wasifanye vyema,”>>> alisema Mwalimu Mkuu. Malalamiko yao wanasema kwamba shule hiyo ilianza kuwa na matokeo mabaya kwenye mitihani ya kitaifa miaka mitano iliyopita, miaka ya nyuma hali ilikuwa poa kabisa.. wazazi hao wamesema wanataka mganga ambaye atawasaidia kufukuza pepo wachafu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: