Shahidi wa nne katika
kesi ya tuhuma za ubakaji inayomkabili Emmanuel Mbasha, mume wa
mwanamuziki wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, jana alidai mahakamani
kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili mlalamikaji.
Hayo yalidaiwa na daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, ambaye alimfanyia vipimo msichana huyo.
Daktari huyo alidai
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba vipimo alivyomfanyia msichana
huyo anayedaiwa kubakwa na Mbasha, havikuonyesha kitu chochote.
Dk. Migole alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa alili ya kufanyiwa vipimo.
Alidai kwamba binti huyo
alipofika hospitalini hapo, alimfanyia kwanza vipimo vya macho kisha
kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, ambavyo hutolewa bure.
Dk. Migole alidai
kwamba baada ya kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, akiwa na
baadhi ya ndugu wa familia yake, hakwenda bali aliingia mitini na
kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.
Alidai baada ya
kufanyiwa hivyo, vipimo hivyo vilionyesha kuwa hakuna kitu chochote
alichofanyiwa, kwa maana ya kubakwa au kuingiliwa na mwanamume katika
mwili wake na kuwajazia fomu aina ya PF3 kwa kile alichokiona.
“Binti huyo hakuonekana
kuwa na ujauzito, maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na wala mbegu za
kiume katika sehemu za siri,” alidai daktari huyo.
Hata hivyo, baada ya
kutolewa ushahidi huo, Hakimu Flora Mujaya, hawakuweza kusikiliza
ushahidi mwingine kutokana na taarifa za msiba wa hakimu mwenzao,
zilizofika mahakamani hapo.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri Aprili 20, mwaka huu.
Mbasha anadaiwa kuwa Mei
23 na 25, mwaka jana, alimbaka binti mwenye umri wa miaka 17, ambaye
anadaiwa ni shemeji yake huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria.
0 comments:
Post a Comment