Waziri wa Kilimo aiomba Marekani Kuboresha sekta Kilimo nchini Tanzania

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeomba nchi ya Marekani kuboresha sekta ya kilimo nchini kufuatia asilimia 90 ya wakulima kutegemea kilimo cha jembe la mkono. Akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childdress Waziri wa Kilimo na chakula na Ushirika Stephen Masatu Wasira amesema kwamba sekta ya kilimo nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo zana duni huku wakulima wadogo katika kilimo hicho wakitumia jembe la mkono suala ambalo ni gumu kuondoa umaskini kwa wakulima hao hasa wa vijijini. Ameongeza kuwa jembe la mkono hutumiwa wakulima wengi wa vijijini katika uzalishaji wa mazao katika Taifa letu suala ambalo linapelekea wao kushindwa kujikwamua kiuchumi. Katika mazungumzo hayo ameiomba serikali ya Marekani kusaidia kuwekeza zaidi katika viwanda vya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu ili waweze kufaidika na juhudi zao na mwishowe waondokane na umasikini . Uwekezaji katika viwanda vya kilimo utasaidia kuepukana na tabia ya kusafirisha malighafi na hivyo kutaongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: