Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia wapiga ramli chonganishi wapatao 225 waliokamatwa kupitia operesheni maalumu katika mikoa ya Tabora, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Katavi, Kagera na Rukwa. Huku Kati yao waganga 97 tayari wamekwisha fikishwa Mahakamani.
Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Bulimba amesema kwamba wapiga ramli hao wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali likiwemo kosa la kukutwa na vifaa ambavyo ni nyara za serikali pamoja na kufanya shughuli za uganga bila kibali.
Katika hatua nyingine jeshi la Polisi limetoa wito kwa mashirika ya dini ,asasi za kiraia, wanahabari kuendelea kuelimisha jamii kuachana na vitendo vya mauaji ya albino vinavyo endelea nchini Tanzania ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya Taifa
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment