WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE WAKABIDHIWA MRADI WA MAJI DC MWAKALEBELA AZUNGUMZIA;

Serikali ya kijiji cha Mdandu Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe mapema march 7 mwaka huu imekabidhiwa mradi wa maji Toka Kanisa la Lutherani Kidugala Dayosisi ya Kusini Chini ya Ufadhili wa serikali ya ujerumani ambao utasaidia kupunguza adha ya maji katika kijiji hicho Kwa Takribani Asilimia 50. Akizungumza na waandishi wa habari Mara Baada ya Kupokea Mradi Huo Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Fredrick Mwakalebela Alisema Kuwa Gharama za Mradi Huo Zinafikia Takribani Shilingi Milioni 85 Jambo Litakalo Saidia Kupunguza Adha ya Maji Safi na Salama Kwa Wananchi. Alisema Kuwa Kutokana na Kupatikana Kwa Mradi Huo Kila Kiongozi Anapaswa Kuwa Mlinzi wa Vyanzo Vya Maji na Kuutunza Mradi Huo Ili Uweze Kuwasaidia Katika Maisha Yao. Katika Hatua Nyingine Alisema Kuwa Kutokana na Idadi ya Ongezeko la Watu Katika Kijiji Hicho Waliokuwa Wakipata Huduma ya Maji Toka Asilimia 50 Hadi 70 ya Sasa Itasaidia Kupunguza Uhaba wa Maji Hayo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: