Ruvuma wahamia Digitali

Mkoa wa Ruvuma umeingia katika mfumo wa digitali kufuatia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini – TCRA kuzindua mitambo ya kurushia matangazo ili kuendana na mfumo wa kisasa wa mabadiliko ya sayansi na teknolojia . Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Habbi Gunze amewaagiza watoa huduma za usambazaji wa visimbuzi walioko mjini Songea kuhakikisha wanakuwa na visimbuzi vya vya kutosha ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji. Naye mkuu wa mkoa wa Rvuma Said Mwambungu ameipongeza TCRA kwa kuzindua mitambo ya kurushia matangazo kwa mfumo wa kidigiti mkoani humo na kusema kuwa hatua itaharakisha maendeleo. Kwa upande wa baadhi ya Wananchi mkoani humo wakiongea na mwakilishi wa mtandao wa Hivisasa wamesema kwamba uamuzi wa serikali kuhamia digitali ni mzuri lakini kuna changamoto nyingi ikiwemo wananchi wa kawaida kushindwa kulipia gharama za kila mwisho wa mwezi pamoja na visimbuzi hivyo kuonesha picha isyokuwa na ubora.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: