Rich Mavoko apata msimamizi wa kazi zake Kenya

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko, amekiri kuibiwa sana kazi zake nchini Kenya, ambapo ilifika kipindi kuna mtu alienda kujitambulisha kama meneja wake na kuweza kuchukua hela za usimamizi wa kazi zake nchini humo. Akihojiwa amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi wa kusaini mkataba na kampuni ya Kaka Empire, ambayo ipo chini ya mwanzilishi rapa Rabbit, baada ya kubaini kuwa ana mashabiki wengi nchini Kenya, na kuna watu wamekuwa wakifaidi kwa kuuza kazi zake bila yeye kufahamu. Ameongeza kuwa baada ya kupata ushauri aliona ni vema aufanyie kazi ushauri huo ingawa asilimia fulani atakuwa anagawana nao akaona sio jambo baya kuliko kupoteza fedha zote.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: