Banza Stone: Ni kweli naumwa ila sijazidiwa

Mwanamuziki wa dansi Ramadhani Masanja ‘Genelali Banza Stone’, amekiri kutozidiwa kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikimuandika vibaya ingawa ni kweli anaumwa lakini sio kwa hatua ambayo vyombo hivyo vinavyotoa taarifa. Akizungumza na Hivisasa Blog nyumbani kwake amesema kuwa ni kweli alikuwa anaumwa na kuongeza kuwa hata sasa anaumwa sana kichwa ambacho kinapelekea kupata kizunguzungu na kuishiwa nguvu. Amesema kuwa kwa mujibu wa madaktari wanadai kuwa maumivu hayo ya kichwa yametokana na kushambuliwa na fangasi sehemu ya kichwa na hivyo kumfanya kuwa na hali ambayo mara nyingi imekuwa ikimkuta ya kupoteza fahamu ama kupata kizunguzungu. “Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri, sio kama hali ilivyokuwa wiki iliyopita na kitu ambacho kinaniuma ni baadhi ya wanahabari kuniandika vibaya kuwa nipo hoi ingawa ni kweli naumwa lakini sijafika hatua hiyo ambayo watu wanadhani,” alisema Banza Ameongeza kuwa bado anapata matibabu ambapo kuna daktari anayemhudumia nyumbani kwao ambapo pia kuwekewa madrip na hivyo hali yake kuanza kutengamaa. Aidha amewaomba watanzania kwa ujumla kumuombea kwa wema apone na kuacha kutunga habari ambazo hazina ukweli wowote kama ambavyo baadhi ya wanahabari wanavyosambaza habari za uongo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: