Mage naye alijikokota hadi
kituo cha daladala kutafuta usafiri wa Bajah
“Anti twende dereva wa bodaboda alimwambia.. .
“Nataka Bajaj, hakuna Bajaj hapa?”
SONGA NAYO SASA . ………..
“Bajaj saa hizi wameshaondoka zao ,
twende na bodaboda ,” alisema kijana
mmoja huku wenzake nao wakijaribu
bahati zao kwa kumwita Mage akapande
bodaboda zao .
“Sitaki, ” alijibu kifupi huku akisimama
kituoni kuangalia usafiri mwingine. Mara ,
Bajaj ilitoka upande wa Moroco ,
akaisimamisha na kupanda .. .
“Kimara.”
“Poa. ”
Njiani, Mage alianza kumsimulia dereva wa
Bajaj jinsi alivyomuoga kupanda
bodaboda. ..
“.. .tena nahisi hiyo siku nitakayopanda
bodaboda nitaanguka mwenyewe bila
kuangushwa ,” alisema Mage…
“Anti hata mimi nakuunga mkono , unajua
wale madereva wa bodaboda
hawajitambui, wanachojua wao ni kwenda
mbele tu lakini sheria za barabarani
hawana habari nazo ,” alisema suka huyo .
Mazungumzo yalichanganya mpaka
wanafika Kimara ambako Mage
alimwelekeza anapotakiwa kushuka … “Haya
asante sana suka, ” alisema Mage baada ya
kulipa, akaingia ndani kwake.
Mage amekuwa mtu wa kuogopa bodaboda
tangu shoga yake, Shungi alipopata nayo
ajali akavunjika mguu na mkono mpaka
sasa hayuko sawasawa. Hali hiyo ilimfanya
Mage aape kwamba siku atakayopanda
bodaboda lolote lile limpate na liwe
fundisho kwake na kwa wengine .
Mara zote inapotokea anataka kwenda
mahali alitumia usafiri wa Bajaj , sanasana
kama yuko sawa alitumia teksi lakini pia
daladala ulikuwa usafiri wake mkubwa .
Wiki moja ilipita, ikafika siku ya kikao
kingine cha ile harusi , kulekule Kinondoni .
Mage alijiandaa, siku hiyo alichelewa
kidogo hivyo saa kumi na moja ndiyo
alikuwa anatoka nyumbani .
Pamoja na kuchelewa huko , Mage
alilazimika kupanda Bajaj badala ya
bodaboda kama alivyoshauriwa na mdogo
wake, Joyce kwamba kwa sababu
amechelewa angepanda bodaboda ili
awahi.. .
“Joy , mimi tangu lini nimepanda
bodaboda, umesahau ya Shungi ?”
“Wewe dada Mage bwana , kwani ajali si
ajali tu ! Hujawahi kusikia mtu amepata
ajali ya Bajaj ?”
“Inatokea Joy lakini si kama ya bodaboda,
bodi ni mwili wako .” Walicheka wote , Mage
akaondoka zake ndani ya Bajaj kuelekea
kwenye kikao.
Kilikuwa ni kikao cha mwisho siku hiyo
ambapo ilitakiwa kila mtu apangiwe
majukumu kwa hiyo kilichukua muda
mrefu sana .Mpaka saa sita juu ya alama
usiku ikielekea siku nyingine , walikuwa
bado wapo kikaoni.
Saa saba kamili ndiyo walianza
kutawanyika huku Mage akiwaza namna ya
kutafuta Bajaj usiku huo , aliamini anaweza
asipate…
“Jamani mwenzenu leo sijui kama nitapata
usafiri, ” Mage aliwaambia wajumbe wa
kikao wakati wakitoka.. .“ Usafiri mbona wa
kumwaga tu. Dar huwezi kukosa usafiri
hata kidogo , ” alisema mjumbe mmoja ,
mama Saida.
Mara , mvua ilianza kunyesha kwa mbali,
Mage na wenzake wakakimbilia kwenye
upenu wa nyumba kujificha .Mvua haikuwa
kubwa wala ndogo, kati kwa kati kiasi
kwamba, mama Saida alisema si mvua ya
kukatika haraka …
“Jamani kwa usiku huu , hii mvua haikatiki .
Hii mpaka kunakucha. Afadhali twendeni,
si tunakwenda majumbani mwetu ?”“Ni
kweli ,” wengine waliunga mkono ,
wakaingia kwenye mvua.
Kila mjumbe alipanda bodaboda , Mage
alisita kwani alijua na mvua ile na akili za
madereva wenyewe ndiyo kabisaaa ! Ajali
nje nje !
Ilifika mahali kukawa kumetulia kabisa ,
Mage akajikuta anabaki peke yake baada ya
bodaboda moja iliyokuwepo kituoni hapo
kuanza kuondoka …
“Anko .. .anko please ,” Mage alimwita
dereva huyo .. .
“Nipeleke Kimara mara moja . ”
“Elfu kumi anti, si unaona mvua hii !”
“Poa, lakini endesha polepole ,” alisema
Mage huku akipanda. Hakuwa na namna
kwani mvua nayo ilichanganya vibaya
sana. “Suka .. .suka , unaona hapo mbele
pana tuta, polepole bwana ,” alisema Mage
huku macho yakiwa mbele kama yeye
ndiye dereva .. .
“Nimeona anti. Usiwe mwoga. ”
“Nisiwe mwoga wakati maisha yangu
nayaona yapo hatarini, we vipi?”
“Anti kwani unadhani naweza
kukuangusha?”
“Kwa jinsi ninavyokuangalia hushindwi .”
“Basi we ngoja nikuoneshe jinsi ya kukaa ili
usiogope,” alisema suka akiweka pembeni
bodaboda yake.
Mage alikaa kuangalia pembeni , ile mikao
ya wanawake wengi kwenye pikipiki au
baiskeli. Suka akamwelekeza akae kama
mwanaume amwangalie yeye. ..
“Yeah ! Kaa hivyo, halafu nishike kiuno ili
ujisapoti .”
Mage alizungusha mikono yake na
kuikutanisha mbele kwenye tumbo la
dereva huyo .. .
“Hapohapo , sasa utaona kama utaogopa .
Unajua nyie wanawake mkipanda pikipiki
huku mnaangalia pembeni ni rahisi sana
kuangukia upande mwingine , lakini hapo
sasa huwezi kuanguka, ” alisema suka huku
akiongeza mwendo wa bodaboda .
Mage aligundua ni kweli yuko salama kwa
mkao huo kuliko ule wa mwanzoni . Kadiri
spidi ya pikipiki ilipozidi , yeye alimlalia
suka mgongoni na kukaza mikono
kumkumbatia na hali hiyo pia ilimfanya
akwepe manyunyu ya mvua na kuhisi kajoto f’lani hivi.. .
Alijikuta akipeleka mikono hadi kuanza kushikashika flaizi .. .
“Hee!” suka alipiga ukelele wa
uendawazimu wa kidereva wa bodaboda …
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment