LULU MICHAELI ADAIWA KUPENDA MAKUBWA KULIKO UWEZO WAKE KATIKA TASNIA

Sidhani kama kuna producer apa bongo mwenye kifafa cha akili, ambaye ataweza kumlipa LULU mil 15 kwa movie moja tu. Ki Ukweli hakuna movie yeyote aliyowahi kuigiza LULU na kuweza kuvunja rekodi ya mauzo kuliko filamu nyingine yoyote hapa nchini na kuweza kuwashawishi ma producer kuweza kumtumia kwenye movie zao ata kwa dau la mil 5 tu. Nina uhakika LULU anaweza kuongoza kwa mauzo ya magazeti ya udaku apa nchini, ila sio kwenye filamu za kibongo, huo ndio ukweli. Siwezi kumlipa Shamsa ford (CHAUSIKU) laki Mbili na nusu kwenye movie ya CHAUSIKU then nikamlipe LULU mil 10 akaigize FOOLISH AGE, that is foolish. Ni upuuzi kumlipa RIYAMA ALLY laki tatu kucheza filamu ya FUNGU LA KUKOSA nikamlipe LULU mil 6 kucheza movie ya FAMILY CURSE. Ni laana kumlipa ODAMA (Jennifer kyaka) laki tatu kucheza filamu ya ODAMA ukamlipe LULU mil 8 kucheza movie ya FAMILY DISASTER. Hakuna awezaye kumlipa NISHA (salma jabu) laki moja na nusu kucheza filamu ya ZENA NA BETINA ukamlipe LULU mil 20 kucheza movie ya HOUSEBOY. Simaanishi kuwa LULU sio muigizaji mzuri ila kiwango chake kwenye tasnia ya filamu bado sana , she has a long way to go, asifananishe umaarufu Wa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii na kiwango cha uigizaji wake kwenye tasnia ya filamu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: