Kada wa Chadema ambaye pia ni ofisa mshuri wa masuala ya Uchumi na Biashara Fredrick Fussi ametangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Songea Mjini kupitia Chama Cha Chadema katika uchaguzi mkuu unataorajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Fussi akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Hotel ya Agopal mjini Songea Mkoani Ruvuma amesema ameamua kutangaza nia ya kutaka kugombea jimbo hilo akiwa na lengo la kutaka kurudisha umiliki wa Halmashauri ya manispaa ya Songea mikononi mwa wananchi wenyewe kwa kuwashirikisha kwenye miradi mbalimbali ya utekelezaji.
Alisema kuwa matamanio ya wapiga kura ni kutaka kuitambua Halmashauri yao jinsi inavyoweza kuwasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na huduma za jamii katika kupunguza baadhi ya matatizo yanayowakabili wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumzia utendaji amesema katika utendaji wake atazingatia mahitaji ya makundi yote ndani ya jamii ikiwemo kufuatilia fedha za miradi mbalimbali ambayo baadhi ya wananchi walidai kuwa imekuwa ikitekelezwa kwa viwango vya chini kwa baadhi ya miradi kushindwa kukamilika.
Kwa upande wa mapungufu amesema licha ya kuwepo na mapungufu ya kiutendaji ndani ya manispaa hiyo bado kumekuwepo na tatizo la miundo mbinu ya barabara pamoja na usafi wa mazingira ambao umeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo.
Akipata ridhaa amesema atajitahidi kutengeneza fursa za ajira hasa kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya vijana na akina mama.
Katika hatua nyingine Fussi ana elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya Uchumi na uongozi wa siasa ambayo aliipata kwenye chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment