Watu sita wafariki kwa ajali moto Dar es salaam

Ilala, watu sita wamefariki dunia kwa ajali ya moto iliyotokea katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana.Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni pamoja Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ). Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kuwa moto huo ulizuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na mstaafu huyo wa Jeshi, David Mpira anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60 jana saa 10:30 alfajiri. Aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa marehemu, Selina Yegela anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50 na 55, ambaye pia ni mstaafu wa iliyokuwa Kampuni ya Kuhudumia Ndege (DAHACO), sasa Swissport. Aidha, moto huo pia umesababisha vifo vya watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 30 ambao ni, Lucas Mpira na Samwel Yegela. Kamanda Nzuki alisema wajukuu wa marehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao ni Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Tumaini iliyopo Kitunda. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ambapo hadi sasa maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na uchunguzi bado unaendelea.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: