SIMBA YAIFUNDISHA SOKA POLISI, MAGURI ANG’ARA

Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Moro katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Simba ilifanikiwa kufunga bao katika kila kipindi huku ikionyesha soka safi. Bao la kwanza katika kipindi cha kwanza lilifungwa na Ajibu ambaye awali alipoteza nafasi nzuri ya kufunga. Polisi hawakuwa walahisi kwa kuwa walionyesha soka safi lakini nao hawakuwa makini katika umaliziaji. Kipindi cha pili, Elius Maguri aliyeisumbua sana safu ya ulinzi ya Polisi aliifungia Simba bao la pili na kuwavunja nguvu Polisi. Simba walionekana kuwa si wale kwani waliendelea kushambulia hata mwisho wa kipindi cha pili. Hata hivyo, Polisi walikuwa wakijibu mara kadhaa lakini safu ya ulinzi ya Juuko Murishid ilipambana kuondoa hatari zote.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: