Serikali yazidi kuzibana shule Binafsi
Bungeni Dodoma, Serikali kupitia wizara ya Elimu na Ufundi imesema itazifutia usajili shule zote za serikali au binafsi, zitakazobainika kukaidi agizo la wizara hiyo lililotolewa wiki iliyopita la kuacha kuweka viwango maalumu na tofauti za ufaulu, ambapo kiwango cha serikali ni alama 30.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa wizara hiyo, Anne Kilango alisema wizara hiyo inaendelea na uchunguzi na kufungia shule zote hata kama zinamilikiwa na wabunge wanatakiwa kufuata sheria.
Aidha, Kilango alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliyetaka kujua hatua za serikali kwa shule zinazoendelea kukaidi agizo hilo.
Akijibu swali hilo, Kilango alisema Wizara baada ya kutoa onyo wiki iliyopita haitatoa nyaraka tena, bali itafanya uchunguzi na kufutia usajili shule zote zitakazokaidi hata zikiwa za wabunge.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment