Kocha Mkuu wa Prisons, David Mwamwaja amesema ana uhakika Yanga watahadithia kuhusiana uwezo wa Prisons watakaporejea jijini Dar.
Yanga wako mkoani Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sokoine.
Mwamwaja amesema wana uwezo mkubwa wa kushinda mechi dhidi ya Yanga hata kama itakuwa ngumu.
“Kweli tunawaheshimu Yanga kama timu kongwe, lakini wanajua uwezo wetu na wanatambua ugumu watakapokutana na sisi.
“Safari hii tunataka kushinda na kubakiza pointi tatu Mbeya. Nakuambia wakirudi Dar watawaeleza kazi ilivyokuwa.
“Tumejiandaa vilivyo na tunajua namna pointi tatu zilivyo muhimu kwetu. Hatuwezi kufanya utani,” alijigamba Mwamwaja ambaye kikosi chake kimekuwa na mwendo wa kusua, hali iliyosababisha mashabiki kuanza kupiga kelele wakitaka afukuzwe.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment