MOTO mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 asubuhi leo wakati wanafunzi wakiwa wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz ,kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, Inspekta Kennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali zilizoko katika bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi kufika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa na hitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo.
Komba alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa waliondoka mjini Iringa ambapo ni zaidi ya kilometa 20 hadi ilipo shule hiyo ili kwenda kuzima moto huo.
Hata hivyo aliwapongeza wananchi kwa moyo wa ushujaa kujitolea kuzima moto huo na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapojitokeza
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment