MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA CCM NEC KWA WILAYA YA LUDEWA ELIZABETH AUGUSTINO HAULE AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 5/02/2015 KATIKA HOSPITARI YA WILAYA YA LUDEWA
Aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Taifa(NEC) wilaya ya Ludewa Bi.Elizabeth Augustino Haule amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 5 februal 2015 katika hospitari ya wilaya ya Ludewa alikokuwa amelazwa tarehe 4 Februal 2015.
Enzi za uhai wake aliweza kuwa muhimili mkubwa kwa vijana ambapo amewahi kuwa katibu wa kikundi cha sanaa cha WUSHU group na baadae kuwa katibu wa IVA YOUTH GROUP na hatimaye kuwa mjumbe wa NEC hivyo mpaka mauti yanamfika amekuwa akitumikia ukatibu wa Iva youth group na Mjumbe wa NEC.
Marehemu Elizabeth alilazwa jana katika hospitari ya wilaya ya Ludewa majira ya saa 5 asubuhi akisumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo yamesababisha kuchukua uhai wake.
Aidha Mbunge wa jimbo la Ludewa kwa chama cha mapinduzi Mh.Deo Filikunjombe ameshtushwa na taarifa hiyo hivyo amewataka wanaccm wilaya ya Ludewa kuwa watulivu kwa kipindi hiki wakati taratibu nyingine kutoka kwa viongozi wa chama zinafanyika
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment