MAHAKAMA:MARUFU KU GOOGLE,YAHOO,MICR OSOFT KUONYESHA MATANGAZO YA KUWAPIMA WAJAWAZITO

Mahakama kuu nchini India imeamrisha kampuni kubwa za internet, Google, Yahoo na Microsoft kubana matangazo ya biashara ya kuwapima wanawake wajawazito ili kubaini jinsia ya mtoto kabla ya kuzaliwa. Matangazo kama hayo, ni kinyume na sheria nchini India kwa sababu kuna visa vingi vya wanawake kutoa mimba wanapogundua wana mtoto mwenye jinsia wasioitaka. Hali hii imechochea tatizo la pengo katika jinsia moja kuwa ikilinganishwa na nyingine. Mahakama ilikuwa inatoa uamuzi katika kesi iliyowasilishwa mbele yake kuhusu kuzagaa kwa matangazo ya biashara ya kubaini jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwenye mitandao hio.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: