Lulu afunika kila idara mpaka kwenye ‘kitabu’

Msanii wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa sasa ameamua kupiga kitabu, anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni, Posta jijini Dar. Alisema mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake. “Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu, anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,”alisema mwanafunzi wa chuo hicho
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: