JK:Tanzania inaongoza kwa kuwa na vyombo vingi vya Habari

Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Duniani zenye vyombo vingi vya habari yakiwemo magazeti. Kauli hiyo ilitolewa na Rais wakati akijibu swali lililokuwa linahoji kwa nini Serikali imesitisha uingizaji wa gazeti la “The East African” wakati wa mkutano wake Rais Kikwete na Rais wa Ujerumani Joachim Gauck. Pia aliongeza gazeti hilo alikufuata utaratibu na sheria na taratibu za nchi ndio maana Serikali imekutana na wahusika ili kuweza kuwaeleza nini cha kufanya. Rais Kikwete aliyataja magazeti yanayomilikiwa na Serikali ambayo ni Daily News na Habari leo huku wagazeti ya watu binafsi ni mengi kama Nipashe,majira,Mwananchi,The Guardian,The Citizen na mengine mengi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: