Huu ni ukatili namba moja kwa wanandoa duniani! Bado picha haijatoka kichwani kwa wakazi wa Manzese jijini Dar kufuatia kifo cha kuchinjwa cha Josephine Ndengaleo Mushi kinachodaiwa kufanywa na mume wake wa ndoa, Remy Joseph (35). Tukio hilo la kutisha kusimuliwa achilia mbali kuona, lilijiri saa 9: 10 alasiri ya Januari 29, mwaka huu ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya Hotel Friend’s Corner Ltd iliyopo Manzese Argentina, Dar. Baada ya habari za mauji hayo kusambaa kama moto wa kifuu, waandishi wetu walianza kuichimba habari hii kwa kina. Kwa mujibu wa mhudumu mmoja wa hoteli hiyo, Januari 28, mwaka huu, Remy na Josephine walifika kwenye hoteli hiyo na kuchukua chumba. Walionekana wenye amani, kwani hakuna sura iliyoonesha kuna tatizo. “Walikuwa kama wateja wengine. Tena niliwauliza kama wanatoka mkoa, wakasema ni wakazi wa Dar es Salaam, wao ni mke na mume kwa ndoa, waliamua kulala hapa ili kuimarisha mapenzi yao, si lazima kila siku nyumbani,”alisema mhudumu mmoja. Kwa mujibu wa baadhi ya wahudumu wa hoteli hiyo, siku ya pili, muda wa saa tisa alasiri, walishtuka kuona damu nyingi ikitoka ndani ya chumba walichopanga wawili hao. “Tulishtuka sana. Tukajua kuna kitu kikubwa kimewapata. Ilibidi tuwagongee mlango ili tujue kilichowapata lakini mlango haukufunguliwa,”alisema mhudumu mwingine. Kwa vile ukimya ulitawala ndani ya chumba hicho huku damu zikiendelea kutiririka, ilibidi uongozi wa hoteli hiyo yenye sifa ya ulinzi, uwasiliane na Kituo cha Polisi cha Ndugumbi ambacho kipo jirani.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: