Diamond, Fally Ipupa kuja na collabo kabla ya March, 2015

Nyota wa muziki wa bongo flava ambaye pia ni rais wa muziki huo, Diamond Platnumz anatarajia kuachia nyimbo nne kwa pamoja kabla ya mwezi March 2015ikiwepo collabo yake na mkali kutoka nchini DRC Congo, Fally Ipupa. Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kuwa ziara ya Diamond barani Afrika imekuwa na mafanikio baada ya kukutana na wasanii wakubwa barani humu kama P-Square, Fally Ipupa,Flavour na wengine kitu kilichomfungulia milango hivyo kuweza kupata nafasi ya kufanya collabo na Fally Ipupa. Aidha Babu Tale amesema kuwa kabla ya mwezi March mwaka huu watakuwa wameshaachia audio nne za Diamond ikiwepo collabo hiyo aliyofanya na Fally Ipupa. Katika hatua nyingine Tale amesema kuwa baada ya kuachia nyimbo hizo video zitafuata na itajulikana zitafanyika wapi kama ni hapa kwa Adam Juma, GodFather au Moe Mussa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: