Zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha hasara kubwa ambayo thamani yake bado haijajulikana.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu ametoa saa 24 kwa wataalam kuhakikisha wanayaondoa maji ndani ya makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile amemwambia mkuu huyo wa mkoa alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kuwa zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko hayo lakini kumetokea uharibifu mkubwa wa mali na vyakula.
“Mvua kubwa zilizonyesha jana usiku zimeshababisha mafuriko haya…tatizo kubwa mji wetu hauna mifereji ya kupeleka maji baharini…athari ni kubwa sana,”alisema Ndile.
Aliongeza kuwa“Mitaa ya Magomeni, Chuno, Kiangu, Skoya,Kisutu Nabwada ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na tatizo hili”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment