MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi ametaka mazuri yaliyofanywa na serikali ambayo ni mengi yatangazwe.
Alisema hayo wakati wa mkutano uliowakutanisha Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa.
“Mazuri ya Serikali ni mengi sana ni lazima yasemwe Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya mengi mazuri lakini hayasemwi, ifike wakati mazuri ya Serikali lazima yasemwe. “Kama kuna mtu ambaye anadhani serikali haijafanya lolote katika kuwaletea wananchi wake maendeleo huyo atakuwa ana lake jambo ” alisema Ndejembi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment