Vanessa Avunja Ukimya, amtambulisha Jux tamasha la Tigo Kiboko yao

Vanessa Avunja Ukimya, amtambulisha Jux tamasha la Tigo Kiboko yao Mwanamuziki aliyeripotiwa sana na vyombo mbalimbali vya habari hasa mitandao ya kijamii kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Jux, Vanessa Mdee usiku wa kuamkia leo amevunja ukimya alipoamua kuwatambulisha mashabiki shemeji yao ambaye naye pia ni mwanamuziki anayefahamika kama Jux. Katika tukio hilo hali ilikuwa hivi, Vanessa Mdee alipanda jukwaani na kuwapa mashabiki makamuzi ya nguvu kwa kuimba nyimbo zake zinazobamba hivisasa katika vituo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi. Nyimbo alizoimba ni pamoja na “Come over” ambayo alicheza kwa ustadi mkubwa suala linalo onesha Vanesa Mdee amejipanga katika kuhakikisha kwamba anakata kiu ya mashabiki wake Aidha, Vanesa(Vee money) alimkaribisha mwanamuziki Barnaba aliyemshirikisha katika wimbo wake mpya unaojulikana kama Siri. Wimbo huo ndio ulikuwa wa mwisho ambapo kabla ya kutoka jukwaani Vanessa aliwaambia mashabiki wake nimlete nani? Mashabiki wakaitikia kwa sauti kubwa Juxiiiiiiiiiiii!!!!! Shemeji yetu!! Baada ya mashabiki kutamka wanamtaka Jux Dj hakufanya ajizi akaupiga moja ya wimbo maarufu wa Jux unaoitwa nitasubiri ndipo akapanda jukwaani na kuanza kutumbuiza. Suala hilo lilionesha kuwa Vanessa amemtambulisha Mwanamuzi Jux kiana kwa mashabiki wake kutokana na kusambaa habari kwamba wana uhusiano wa kimapenzi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: